Friday, August 5, 2011

NIMR YAIFANYIA UTAFITI DAWA YA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI!

Taasisi ya Taifa ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu NIMR imesema mpaka sasa imekwishafanya utafiti wa dawa ya kupunguza makali ya magonjwa nyemelezi yanayotokana na upungufu wa kinga mwilini.

Akizungumza mjini Dodoma katika maonesho ya wakulima “Nane nane” Mkuu wa masuala ya utafiti wa Ki-sanyansi wa taasisi hiyo Dakta JULIUS MASSAGA amesema mbali na kufanya utafiti wa kisayansi wa Dawa hiyo pia NIMR imekuwa ikijihusisha na utafiti wa Dawa za Asili ambao mpaka sasa umetoa matokea mazuri.


Kuhusu dawa ya kupunguza makali ya upungufu wa kinga mwilini Dakta MASSAGA amesema hivi sasa NIMR ipo katika hatua za mwisho za kufanya usajili wa Dawa hiyo ili ianze kuzalishwa kwa wingi na kuwafikia wananchi ambao ni wahitaji wa dawa hiyo.

No comments:

Post a Comment