Wednesday, May 11, 2011

MAKUSANYO YA KODI YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 18 MWAKA JANA!

                                                                       ZITTO KABWE
Kufuatia kuwepo kwa taarifa za kufilisika kwa serikali ziliztotolewa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini ZITTO KABWE, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA Bwana HARRY KITILYA amesema makusanyo ya kodi yameongezeka kwa asilimia 18 kwa mwaka huu wa fedha ikilinganishwa na mwaka uliopita


Akizungumza na kituo hiki mjini Dodoma inakoendelea semina elekezi kwa viongozi wa serikali, KITLYA amesema licha ya kuwepo kwa ongezeko hilo makusanyo kwa kila mwezi yamepungua kwa asilimia saba.


KITILYA amesema matarajio ya TRA ni kukusanya shilingi Bilioni 430 kwa mwezi huku matarajio ya mwaka yakiwa ni kukusanya shilingi Trilioni 5.25.

No comments:

Post a Comment