Tuesday, May 29, 2012

WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WATEMBELEA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)!

Baadhi ya Michoro ilichorwa na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambazo leo wamepata nafasi ya kuonyesha kazi zao tofauti na masomo wanayosomea.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakisalimiana na wenyeji wao wakati walipokuja kwenye maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo wanafunzi waliweza kuonyesha uwezo wao tofauti na masomo wanayosomea.
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akitoa maelezo kwa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa waliokuja Kuona kazi za wanafunzi wa UDOM wakati wanafunzi hao Wakionyesha Uwezo tofauti na Masomo wanayosomea.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliweza pia kupata nafasi ya kutembelea Jengo la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma na kufanya ziara ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati walipokuja Kuangalia maonyesho ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma yanayoendelea Kufanyika Muda huu katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma.
Baadhi ya Wakuu Wa Mikoa na Wilaya walipotembelea Jengo jipya la Utawala la Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).

No comments:

Post a Comment