Tuesday, May 29, 2012

MAONYESHO YA WANAFUNZI UDOM YAFANA JANA KATIKA UKUMBI WA CHIMWAGA ULIOPO CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)!

Muandaaji wa Maonyesho haya Ester Zangi ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesomea shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa na utawala wa umma(Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao Wameonyesha vipaji vyao Vya Kuchora Michoro inayoonekana hapo katika maonyesho yaliyofanyika jana Chuo Kikuu Cha Dodoma katika Ukumbi wa Chimwaga.
Mmoja wa wanakamati wa maandilizi ya maonyesho haya ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 Bi Atu anayesoma shahada ya kwanza ya Mazingira ya Chuo Kikuu Cha Dodoma alipokua akitoa neno wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).
Wanafunzi wa UDOM wanaosoma shahada ya kwanza ya Filamu na Sanaa, Kiswahili wakionyesha uwezo wao wa kucheza boringo katika maonyesho yaliyofanyika jana Katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).

No comments:

Post a Comment