Thursday, June 23, 2011

PAPAA MSOFE ATUHUMIWA KUVAMIA KIWANJA MBEZI BEACH!

                                           Papaa Msofe akiwa na Lady JAY Dee.
Mkazi mmoja wa jijini Dar es salaam ametoa malalamiko yake juu ya baadhi ya polisi wa kati na wale wa chini wa kituo cha kawe, wanaoshirikiana na mvamizi wa kiwanja chake kilichopo Mbezi ya kawe Bw. Marijani Msofe maarufu kama Papaa Msofe, ambaye hapo awali hakuwa amejitokeza kuwa na yeye pia ni mmiliki wa kiwanja hicho.

Edwin Mlay, mmiliki halali wa kiwanja hicho, amesema licha ya sehemu hiyo kuwa na nyumba ya vyumba viwili, matofali zaidi ya elfu sita na uzio mkubwa, Papaa Msofe alithubutu kuagiza watu kuyaondoa matofali yote, kuvunja nyumba yote, na kubadili sehemu ya uzio, na baada ya kuripoti katika sehemu husika, amekuwa akipewa ahadi za mara kwa mara bila ya mafanikio.
Aidha kituo hiki pia kilimtafuta Papaa Msofe anayetuhumiwa kwa uvamizi wa kiwanja hicho, ili kulizungumzia suala hilo ambaye amesema kwamba hausiki na kiwanja hicho na hajawahi kuhusishwa na suala hilo.

3 comments:

  1. Nimeona kwenye jamii forum kwamba huyu Marijani Msofe ni kweli TAPELI la madini na Ardhi na wanadai mpaka hata ITV walimuonyesha. Wanasema kiwanja alichodhulumu hapa alikirudisha tarehe 11/11/2011 kwa huyu Mlay na ITV walionyesha live. Hivi aliporudisha alifanywa nini? Inaonyesha Mapolisi na wizara ya Ardhi wanamtetea na kuwafundisha watu kwamba hii ndio spirit tunayotaka, unakwapua ukiona soo unarudisha unajaribu kwingine! Professor Tibaijuka tupe ufafanuzi tafadhali. Hongera kubwa kwa vyombo vya Habari Makini kama EATV kwakutoa habari zenye uhakika bila kuogopa au kununuliwa na matapeli. Kazi zenu nazikubali.

    ReplyDelete
  2. Mimi maoni yangu serikali yote nayo ni fisadi anzia wizara ya mambo ya ndani ardhi na jeshi la polisi wte ni mafisadi na wako kitu kimoja na uyu tapeli jambazi msofe,kwanini hawakumchukulia hatua yyte uyu bwana kwa kitendo alichomfanyia mlay iko wapi haki tanzania mnasema tunayo haki ? itafika mahali nasisi watu wa chini tutachoka tutajichukulia sheria mikononi ndipo hapo mtapotaman ardhi ipasuke mtumbukie ndani

    ReplyDelete
  3. Hivi watanzania hawajui kwamba Marijani Msofe anatumiwa na ofisi ya magogoni kuendesha uhalifu wake. Labda mageuzi yatokee Chadema wachukue nchi lakini kama uongozi ukibaki huu huu hakuna cha Mama Tibaijuka wala Polisi watakaomsumbua! na bahati mbaya hayuko mwenyewe kuna ndama mtoto wa ngombe ni kitopaz ukipita karibu nae anachanja Papa Msofe hamfikii kwa hela aliyonayo.

    ReplyDelete