Tuesday, June 14, 2011

TGNP YAIOMBA SERIKALI KUFUTA KODI YA VIFAA VINAVYOTUMIWA NA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU!

Serikali imeombwa kufuta ushuru na kupunguza bei ya vifaa vinavyotumiwa na wanafunzi wenye ulemavu nchini kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa Vifaa hivyo.

Ombi hilo limetolewa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, AL-SHAYMAA JOHN KWEGYIR wa CCM wakati alipouliza swali akitaka kufahamu gharama ya vifaa hivyo kwa walemavu wenye mahitaji maalum.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha na Uchumi, MUSTAPHA MKULO amesema serikali italiangalia suala hilo kwa moyo wa huruma .
Hata hivyo , Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika JUMANNE MAGHEMBE ametolea ufafanuzi suala hilo na kusema kuwa vifaa vyote vya kujifunzia kwa walemavu havitozwi kodi.
MAGHEMBE ambaye alikuwa Waziri wa Elimu katika kipindi kilichopita amesema serikali imekuwa ikifanya juhudi kuhakikisha walemavu wanapata vifaa vya kujisomea.

No comments:

Post a Comment