Monday, November 14, 2011

WABUNGE CHADEMA WATOKA BUNGENI KUKATAA KUJADILIWA KWA MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA MPYA!

Wabunge wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, leo wametoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa madai ya kutoafikiana na kile walichodai kuendelea kujadiliwa kwa Muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba wakati ukiwa haujatimiza masharti ya kusomwa kwa mara ya pili na ya tatu kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Kama kawaida, wabunge wa Chadema na wa Nccr Mageuzi wamesusia kikao cha kujadili mchakato wa kuunda katiba mpya na kuamua kutoka nje, mara baada ya Tundu Lisu kuwasilisha mapendekezo ya kambi ya upinzani.

Wabunge hao wametoka mara baada ya Mbunge wa Singida Mashariki na Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria TUNDU LISSU kuhitimisha kuwasilisha maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani bungeni iliyopendekeza kusitishwa kwa mjadala huo ili maoni ya wananchi yakusanywe kwanza.



Ilitolewa mionngozo juu ya hoja kadhaa zilizojitokeza lakini spika alizikataa na ndipo wabunge hao wakaamua kutoka nje na kuacha wabunge wa ccm na wengine kama TLP kuendelea na kuchangia mapendekezo yaliyotolewa na Waziri wa Katiba, Mama Kombani.



Majadiliano yataendelea kesho kama kawaida kwa wabunge kuujadili mswada huo kwa mara ya pili kwa mujibu wa taratibu na kanuni za bunge ambazo zimeonekana kupotoshwa na wanaharakati.

Watu wengi wameelewa kuwa kilichokuwa kifanyike leo ni kujadili muswada wa katiba mpya hivyo usomwe kwa mara ya kwanza ili watu wauelewe na watoe maoni yao, wakati kumbe kinachojadiliwa ni namna ya kuandaa utaratibu wa kuunda hiyo katiba mpya na namna ya watu kupewa nafasi ya kutoa maoni na madukuku yao kuhusu katiba hiyo ijayo!!


Kabla ya Wabunge hao kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge, kuliibuka majibizano baina yao na spika wa Bunge alipompa nafasi Mbunge wa Same Mashariki, ANNE KILANGO MALECELA kuchangia hoja. Wakati huohuo Bunge limepitisha mswaada wa sheria ya manunuzi wa mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment