Monday, May 28, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA VITABU VIWILI VYA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM YUSUPH MAKAMBA


  Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wageni waalikwa na wanachama wa CCM, waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa mujibu wa Biblia, na Kurani Tukufu,  
 Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikata utepe kuzindua kitabu cha Binadamu na Kazi, kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2012, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu.

 
 Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akionyesha Kitabu cha Binadam na kazi baada ya kukizindua kitabu hicho kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2012, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo,Mama January Makamba

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba, wakati wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa vitabu vya Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi na Binadam na kazi, vilivyotungwa na Katibu huyo. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 27, kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam.




 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.



 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.



No comments:

Post a Comment