Monday, June 6, 2011

HAYA YALIKUPITA WEEK END HII JIJINI DAR ES SALAAM....TUNAKUKUMBUSHA!

Vodacom Miss Kurasini Mwajabu Juma akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi, kushoto mshindi wa pili Naifat Ally na mshindi wa tatu kulia Prisca Steven.

Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude akimkabidhi mshindi wa Vodacom Miss Kurasini Mwajabu Juma kiasi cha fedha taslimu cha shilingi 500,000, shindano hilo lilifanyika Jijini Dares Salaam.
Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude, akaiwaaga wachezaji wa timu ya Holy Family ya mkoa wa Ruvuma waliokuwa wakielekea Zanzibar kwenye mashindano ya Muungano Cup watapambana na mshindi wa Zanzibar kesho, kushoto Mratibu wa shindano hilo Daud Yassin. 
Mmoja wa wacheza wa timu ya Holy Family ya Mkoa wa Ruvuma akijaribu kumili mpira mbele ya Afisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na Mratibu wa shindano la Muungano mara baada ya kukabidhiwa mipira kwa ajili ya mchezo wa kesho na timu ya Zanzibar.

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea ya klabu bingwa Tanzania 2011 wakichumpa kwa kuanza mashindano hayo ya kilometa 200, yanayofanyika Funky Obitz Masaki na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Mmoja wa washiriki wa shindano la kuogelea la klabu bingwa Tanzania 2011 akijitahidi kumaliza kilometa 200 katika shindano hilo linalofanyika Funky Obitz Masaki na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Warembo tano bora waliofanyikiwa kuingia katika shindano la kumtafuta Vodacom Miss Kurasini ambapo Mwajabu Juma (9) ndiye alienyakua taji hilo.

MASHINDANO YA MBIO ZA KUOGELEA MITA 100 YALIVYOKUWA DSM!

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akimvalisha medali mshindi wa kuogelea mita 100 katika mashindano ya klabu bingwa Tanzania kwa washiriki chipukizi Agnes Kimimba.
Waogeleaji wa  timu ya KMKM kutoka Zanzibar kutoka kushoto Ally Hamiss,Omary Abdallah na Othman Ally wakibusu medali zao za dhahabu mara baada ya kutangazwa washindi wa klabu bingwa Tanzania kwa upande wa watu wazima,mashindano hayo  yamefanyika  Funkys masaki jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Katibu Mkuu wa TSA Noel Kiunsi akiwaangalia waogeleaji Ankitu Bhatt(15)na Macayla Buchanan(15)wa timu ya Stingray klabu ya jijini Dares Salaam wakishangilia ushindi wao  mara baada ya kutangazwa washindi wa kuogelea katika mashindano ya klabu bingwa Tanzania kwa waogeleaji chipukizi,mashindano hayo yalifanyika Funkys jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Katibu Mkuu wa TSA Noel Kiunsi(kushoto)na Ofisa mkuu mwendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia wakiwakabidhi kombe timu ya KMKM kutoka Zanzibar waliochukua ushindi wa mashindano ya klabu bingwa Tanzania kwa upande wa watu wazima,Mashindano hayo yalifanyika Funkys jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Ofisa Mkuu mwendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Correia akiwakabidhi kombe wachezaji wa timu ya kuogelea ya KMKM kutoka Zanzibar kushoto Hanna Ally na Othman Abdallah baada ya kuwa washindi wa jumla wa mashindano ya klabu bingwa Tanzania,Mashindano hayo yalifanyika Funkys jijini Dares salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

JESHI LA POLISI LASEMA HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA!

                    Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini, PAUL CHAGONJA
Jeshi la Polisi nchini limesema hakuna aliye juu ya sheria nchini hivyo kitendo cha kumkamata na kumshikilia kwa muda wa siku mbili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema FREEMAN MBOWE kimetokana na amri iliyotolewa na mahakama.

Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini, PAUL CHAGONJA amesema wao kama jeshi la Polisi hawana ugomvi na Chadema na walichokifanya ni kutekeleza agizo la mahakama baada ya MBOWE kushindwa kufika mahakamani jijini Arusha kuendelea na kesi inayomkabili.
Aidha kikosi cha kudhibiti dawa za kulevya cha jeshi hilo kinawashikilia watu nane kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya akiwemo Mfanyabiashara MWANAIDI RAMADHANI maarufu kama MAMA LEILA anayetumia Sura sita tofauti kwa lengo la kuwalaghai wananchi.

SERIKALI YATAKA JAMII ISHIRIKI KAMPENI KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO!

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA, SOPHIA SIMBA na wadau wengine wakizindua mpango huo leo hii.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA akipanda kwenye moja ya pikipiki itakayotumika kwenye vituo vya afya wakati wa utekelezaji wa mpango huo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA akiwa na baadhi ya wanafunzi walioshiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuzuia vifo kwa watoto na akina mama wajawazito.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, DKT. HADJI MPONDA, ameitaka jamii kushiriki katika kampeni ya kupunguza vifo vya Wanawake wajawazito na Watoto nchini, kufuatia asilimia 28 ya vifo vya wanawake kusababishwa na kutokwa damu nyingi wakati kujifungua.



Akizindua Kampeni hiyo, Waziri MPONDA, amesema tafiti za mwaka 2010 zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la Wanawake wanaojifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 47 hadi 50 na kwamba mpaka sasa zahanati 478 na vituo vya afya 78 vimejengwa nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, SOFIA SIMBA, amesema Serikali imeongeza kiwango cha udahili wa wanafunzi vyuoni kwa lengo la kupunguza tatizo la uhaba wa madaktari kwenye vituo mbalimbali vya Afya nchini.

JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA (CCT) YATAKA SERIKALI ISIJIHUSISHE NA MAHAKAMA YA KADHI!

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imeitaka Serikali isijihusishe na suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi hapa nchini isipokuwa suala hilo waachiwe waislamu wenyewe.

Hayo yamebainishwa Jijini DSM na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Askofu Peter Kitula wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na maazimio yaliyofikiwa na Mkutano wa 45 wa Halmshauri kuu ya CCT.
Askofu huyo amesema Serikali inapaswa kujitoa katika suala hilo kwa sababu yenyewe haina dini, ingawa uanzishwaji wa mahakama hiyo ni jambo zuri linalowahusu waislamu hivyo linapaswa litenganishwe na shughuli za Mamlaka ya Uendeshaji wa nchi.

WAKAZI WA MWANANYAMALA KWA KOPA WALALAMIKIA MAJI TAKA!

Baadhi ya wakazi wa Mwananyamala kwa Kopa jijini Dar es Salaam wameilalamikia kampuni iliyopewa zabuni ya kukarabati barabara katika mtaa wao kushindwa kufukia mashimo waliyoyachimba wakati wa ukarabati huo.
Wakizungumza na blogu hiki wakazi hao wamesema mkandarasi huyo alichimba mashimo barabarani ili kuweka kifusi lakini mpaka sasa haonekani na amesitisha zoezi hilo bila kutoa taarifa yoyote.