Wednesday, August 10, 2011

MWILI WA LUTENI JENERALI MAYUNGA WAAGWA LUGALO DAR LEO!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Luteni Jenerali mstaafu , Silas Peter Mayunga, aliyefariki hivi karibuni. Shughuli ya kugwa kwa mwili ya marehemu Mayunga imefanyika leo Agost 10, katika Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwiny, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Shimbo na Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakiwa katika shughuli ya mazishi kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi kwenye Viwanja vya Kambi ya Jeshi Lugalo leo Agost 10.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayungi, wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Viongozi wa Serikali, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agosti 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali staafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Luteni Jenerali, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10.
Waziri Mstaafu, Salim Ahmed Salim, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu Luteni Jenerali mstaafu, Silas Peter Mayunga, wakati wa shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Kambi ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo Agost 10. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Na Mwandishi Wetu
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete leo amewaongoza baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Watumishi wa umma, Ndugu na jamaa kuaga kijeshi mwili wa Marehemu Luteni JENERALI SILAS MAYUNGA aliyefariki Agosti 6 mwaka huu katika Hospitali ya Apollo, New Delhi, nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu tangu Julai 2011.


Baada ya kuuaga mwili huo kwenye kambi ya Jeshi LUGALO Rais KIKWETE aliendelea na majukumu yake mengine ili kupisha shughuli zingine ikiwemo kuagwa tena kifamilia nyumbani kwake Ilala kabla ya kusafirishwa kesho kwenda Mwaswa Shinyanga kwa ajili ya mazishi.


Baadhi ya viongozi akiwemo Luteni Jenerali Mstaafu GIDION FUNDI SAYORE na Waziri Mkuu Mstaafu wamezungumzia utendaji wa Marehemu Luteni JENERALI MAYUNGA enzi za uhai wake.


Baadhi ya viongozi WENGINE waliohudhuria ni Mke wa Rais Mama SALMA KIKWETE, Jaji Mkuu Mstaafu AUGUSTINO RAMADHANI, Rais Mstaafu BENJAMIN MKAPA, VITA KAWAWA na MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM na waziri mkuu wa zamani, DK SALIM AHMED SALIM.


Jenerali Mayunga mbali ya Ofisa wa juu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali, ikiwamo ukuu wa mkoa na Balozi wa Tanzania, Nigeria na Jamuhuri ya Kidemokarsia ya Kongo (DRC). Mayunga atakumbukwa kwa jinsi alivyoongoza mapambano ya vita vya Kagera kumng'oa Nduli Idd Amin mwaka 1978. Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi. Amin.

No comments:

Post a Comment