Monday, June 6, 2011

JESHI LA POLISI LASEMA HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA!

                    Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini, PAUL CHAGONJA
Jeshi la Polisi nchini limesema hakuna aliye juu ya sheria nchini hivyo kitendo cha kumkamata na kumshikilia kwa muda wa siku mbili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema FREEMAN MBOWE kimetokana na amri iliyotolewa na mahakama.

Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini, PAUL CHAGONJA amesema wao kama jeshi la Polisi hawana ugomvi na Chadema na walichokifanya ni kutekeleza agizo la mahakama baada ya MBOWE kushindwa kufika mahakamani jijini Arusha kuendelea na kesi inayomkabili.
Aidha kikosi cha kudhibiti dawa za kulevya cha jeshi hilo kinawashikilia watu nane kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya akiwemo Mfanyabiashara MWANAIDI RAMADHANI maarufu kama MAMA LEILA anayetumia Sura sita tofauti kwa lengo la kuwalaghai wananchi.

No comments:

Post a Comment