Wednesday, October 12, 2011

WAFUGAJI WATAKIWA KUJIKITA KWENYE UFUGAJI WA NG'OMBE WA KISASA!

Wito umetolewa kwa wafugaji nchini kujikita kwenye ufugaji wa Ng’ombe wa kisasa ili waweze kuwa na mifugo bora itakayorudisha tija ya nguvu kazi wanayoitumia katika kuihudumia.

Daktari wa mifugo wa Shamba la mifugo la Chuo Kikuu cha Sokoine SUA Morogoro DK LAMECK MNANA amesema kama wafugaji wataanza kufuga kisasa na kuwapatia ng’ombe virutubisho vyote vinavyohitajika wataongezeka uzito na kutoa faida mara mbili.


Katika hatua nyingine DK MNANA ametoa wito kwa Watanzania wanaohitaji kujifunza ufugaji wa ng’ombe kisasa kufika chuoni hapo ili kupata maelezo ya kitaalam juu ya unenepeshaji mifugo.
                                                                Ng'ombe wa maziwa

No comments:

Post a Comment