Sunday, March 11, 2012

UNAKUMBUKA TUKIO LA TSUNAMI LILILOIKUMBA JAPAN SIKU KAMA YA LEO MWAKA JANA? PATA PICHA TOFAUTI KUHUSU MATUKIO YA SIKU HIYO NA HALI ILIVYO SASA!

PICHA ZOTE ZINAONESHA HALI YA AWALI NA ILIVYO SASA BAADA YA MWAKA MMOJA.

Wakati Japan ikiadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea kwa Tsunami na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa rishta 9, wananchi wamepanga kufanya maandamano makubwa kupinga matumizi ya nyuklia. Maandamano hayo yamepangwa kufanyika, sehemu zote nchini Japan, zikiwemo Koriyama eneo uliopo mtambo wa Fukushima Daichi na kusababisha janga kubwa zaidi la kinyuklia kuwahi kushuhudiwa duniani tangu mwaka 1986, ilipotokea ajali ya CHERNOBYL.


Watu zaidi ya 19,000 waliuawa ama kupotea wakati wa janga hilo lililoharibu pia nyumba zaidi ya 370,000. Hadi sasa, waathirika wa ajali hiyo, bado wanaishi katika makazi ya muda huko Iwate, Miyagi na Fukushima.
Mwaka mmoja baada ya ajali hiyo kutokea kwenye kinu cha nyuklia cha Fukushima nchini Japan, swali linalozuka ni je, umeme unaohitajiwa na nchi hiyo iliyostawi kiviwanda utatoka wapi kwa siku zijazo?


Inashangaza kuona kwamba nchini Japan kila kitu kinakwenda sawa licha ya kwamba sehemu ndogo tu ya umeme wa nguvu ya nyuklia iliyokuwa inatumika zamani ndio inayotumika hivi sasa.
Baada ya janaga hilo, hakuna aliyefikiri kwamba Japan nchi ya tatu kwa utajiri duniani, ingeweza kujimudu bila ya kuwa na umeme utokanao na nguvu ya nyuklia.

ROSE MUHANDO KUUPELEKA UTAMU WA YESU KWENYE TAMASHA LA PASAKA!

                                       Rose Muhando
Na Mwandishi Wetu
MALKIA wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Alex Msama, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Muhando amethibitisha kushiriki tamasha hilo.

"Katika tamasha la Pasaka mwaka huu ndipo Rose Muhando atapata fursa ya kutambulisha albamu yake ya nne ya Utamu wa Yesu ambayo haijawahi kuzinduliwa tangu aikamilishe," alisema Msama. Albamu ya Utamu wa Yesu inabeba nyimbo saba ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawa Sawa.

Msama alisema pia Muhando ataimba pamoja na Anastazia Mukabwa wa Kenya aliyeshirikiana naye katika albamu ya Vua Kiatu, na baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu. "Mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Muhando atakuwepo na Mukabwa atakuja na kundi la waimbaji wake," alisema Msama.

Albamu ya Vua Kiatu inabeba nyimbo nane ambazo ni Vua Kiatu uliobeba jina la albamu hiyo, Ee Mungu, Usiwe Manamba, Nzizilela, Nishike Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme. Mbali na Mukabwa, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho wa Dar es Salaam, kundi la Glorious Celebration na Atosha Kissava kutoka Iringa.

Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu. Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane. Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya. Picha na FULLSHANGWE!

UMATI WA WAFUASI WA CUF WAMPOKEA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO Prof.IBRAHIM LIPUMBA!

Umati wa wafuasi wa Chama cha Wananchi CUF hii leo umejitokeza kumpokea Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa IBRAHIM LIPUMBA aliyekuwa nchini Marekani kwa kazi maalum aliyopewa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuangalia njia bora zinazoweza kutumika katika kurekebisha uchumi wa dunia uliporomoka hususani kwa mataifa yanayoendelea.



Akizungumza Mara baada ya kuwasili, nchini, Prof LIPUMBA amesema kuwa atatumia fursa aliyopata mara baada ya kuteuliwa na umoja huo katika kushauri namna ya kuboresha uchumi wa nchi kufuatia kuwa miongoni mwa mataifa yanayoendelea Ulimwenguni.

ZITTO KABWE ALITEKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI KWA HOJA ZA ARDHI, MAJI NA AJIRA!

                                  Ardhi, Maji na Ajira kuamua Ubunge Arumeru Mashariki.


Na Zitto Kabwe
"Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi mnavyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu". Haya yalikuwa baadhi ya maneno yangu katika hotuba ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kuzindua kampeni za chama chetu katika viwanja vya Leganga katika mji mdogo wa USA River wilayani Arumeru.



Siku moja kabla ya siku ya uzinduzi nilikuwa najisomea makala mbalimbali kuhusu Wilaya ya Arumeru. Pia nilitumia muda mrefu kuzungumza na wananchi wa Meru ili kujua uchaguzi huu una maana gani kwao. WaMeru wengi niliozungumza nao waliniambia namna wanavyochukizwa na ukosefu wa Ardhi kwa wananchi. Baadhi waliniambia kwamba Kama Serikali haitachukulia suala la Ardhi kwa uzito wake Meru kutatokea vurugu kubwa sana.


Vurugu Meru sio Jambo jipya kabisa. Inakumbukwa kwamba miaka ya 1950 kulitokea fujo na wananchi kuchomewa nyumba zao ili kupisha wakulima wakubwa kutoka Afrika Kusini (makaburu) katika eneo la Engarananyuki. Vurugu hizi ndio zilipelekea WaMeru kuchanga fedha kumpeleka ndugu Jafet Kirilo huko Umoja wa Mataifa kutetea Ardhi ya Wameru mwaka 1952 kufuatia vurugu za mwaka 1951. Licha ya juhudi hizo bado Ardhi ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Meru.


Mashamba makubwa ambayo walipewa walowezi wakati wa Uhuru yaligawiwa kwa familia chache sana Meru. Wanasiasa walijipa mashamba makubwa na mengine mpaka Leo hayakugawiwa. Ujamaa na utaifishaji wa mashamba haukufanyika Meru kwa mshangao mkubwa sana na hata mashamba ambayo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliagiza wapewe wananchi walipewa Wabunge, Madiwani, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri (soma Brian Cooksey kuhusu uwekezaji katika Maua, June 2011).


Hivi Leo Ardhi kubwa ya Meru imeshikwa na matajiri na kulimwa Maua. Kilimo hiki cha Maua mwaka 2008 kiliingizia Taifa fedha za kigeni takribani tshs 150bn. Hata hivyo kuna malalamiko makubwa sana ya wananchi wanaofanya kazi katika mashamba haya kuhusu malipo duni na nyenzo za kufanyia kazi. Kuna malalamiko kuhusu kemikali na madawa yanayotumika na afya ya mfanyakazi kutozingatiwa.


Ifahamike kwamba Benki ya Rasilimali Tanzania inasimamia mikopo ya zaidi ya tshs 50bn ambazo kampuni za Maua zilipewa kwa Dhamana ana ya Serikali. Katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, suala hili liliibuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TIB kukiri kwamba hakuna kampuni umeanza kulipa mikopo hii. Ni dhahiri Serikali itajikuta inalipa madeni haya yaliyokopeshwa kwa kampuni binafsi! Hii pia inaonyesha namna amabvyo serikali inafanya haraka na wepesi kusaidia wawekezaji kuliko wananchi wanaoteseka na kukosa Ardhi ya kulima na kujipatia ruziki.
                                                     Wawekezaji wanapewa Ardhi na mtaji!
Haya ndio yanajenga hasira ya wananchi wa Meru. Hasira hii kwa vyovyote itahamishiwa katika sanduku la kura ili kumpata Mbunge kutoka miongoni mwao atakayeweza kusimama kidete kuhakikisha Ardhi inapatikana kwa wananchi wa Meru. Kwa nini huko nyuma, katika chaguzi zilizopita Jambo hili halikuwapa hasira wananchi? Ni dhahiri hapakuwa na Mwanasiasa ambaye ana uwezo mkubwa wa kulieleza na kuwapa imani wananchi. Ndugu Joshua Nassari amedhihirisha kwamba analijua tatizo hili kwa dhati kabisa. Nilivyomsikiliza akiongea katika kampeni, na pia katika mazungumzo yetu binafsi amenithibitishia kuwa ni mwanasiasa kijana mwenye kipaji kikubwa katika kujenga hoja na ku articulate masuala ya msingi.


Changamoto nyingine kubwa kwa Meru ni haki ya kupata Maji. Meru kuna Maji mengi sana lakini matajiri wenye mashamba wameyazuia Maji hayo na hivyo wananchi wa kawaida hawapati Maji ya kumwagilia mazao Yao na pia kwa matumizi ya nyumbani. Hili nalo linajenga hasira kubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Ardhi na Maji ni masuala yanayokwenda pamoja wilayani Meru.


Mwisho kabisa nimeona makundi ya vijana wasio na ajira na hivyo kukosa Kipato. Vijana wengi wanashinda kwenye stendi za mabasi na kuita abiria. Ukosefu wa Ajira kwa vijana Kama tusemavyo kila wakati ni changamoto kubwa sana kwetu viongozi na hasa viongozi vijana. Natumai ndugu Joshua Nassari atahusisha suala la Ardhi na Maji katika muktadha mzima wa Ajira na Kipato kwa wananchi wa Arumeru Mashariki. Uchaguzi wa Arumeru ni uchaguzi kati ya kuwa na Ardhi au kuendelea kutokuwa nayo. Ni uchaguzi muhimu kwa watu wa Meru. Wasio na Ardhi watamchagua mgombea atakayesimamia mgawo wa Ardhi unaozingatia haki. Mgombea huyo ni mgombea wa CHADEMA ndugu Joshua Nassari.
                                                                             Mh Zitto Kabwe.

SERIKALI ITEKELEZE KWA VITENDO MKATABA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU!

                Mratibu wa vikundi vya Pambazuko Klabu wilayani Arumeru, Bi. Vick Kimaro.
                     Mwalimu Philipo Meli wa Shule ya Sekondari Kimyak wilayani Arumeru.
Wanafunzi wenye ulemavu wa Chuo cha Mafunzo kwa Watu wenye Ulemavu Usa River wilayani Arumeru wakifanya mahojiano na mtandao wa The Habari.com
Mwanafunzi Kelvin Bosco (mlemavu wa akili) toka Shule ya Msingi Naurei wilayani Arumeru akiandika ubaoni baada ya kupewa maelekekezo.

 Na Joachim Mushi, Thehabari.com-Arumeru
BAADHI ya waenezi wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu na wafanyakazi walemavu wilayani hapa wameitaka Serikali kuonesha kwa vitendo utekelezwaji wa madhiriano ya mkataba huo ili kundi hilo kuanza kupata haki sawa za kimsingi kama ilivyo kwa watu wa kawaida.


Changamoto hiyo imetolewa hivi karibuni na Bi. Vick Kimaro ambaye ni mmoja wa viongozi wawakilishi wa watu wenye ulemavu wilayani Arumeru, wanaofanya kazi kwa ushirikiano na Kituo cha Habari Kuhusu Walemavu (ICD) cha jijini Dar es Salaam.


Bi. Kimaro ambaye ni mlemavu wa viungo (mguu) alisema licha ya Serikali kuridhia utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu bado maeneo mengi, baadhi ya wananchi na hata viongozi hawatambui uwepo wa mkataba huo, ikiwa ni pamoja na kutojali haki za msingi kwa walemavu.


Alisema kutokana na hali hiyo bado watu wenye ulemavu wamekuwa wakikumbana na vikwazo vingi katika ufuatiliaji wa haki mbalimbali ambazo ni za msingi kwa jamii yote. “...unaweza kujiuliza kama tayari kuna mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu ambao Serikali imeridhia kwanini tunaendelea kukubwa na vikwazo kwenye huduma anuai za msingi?,” alisema Bi. Kimaro.


“Pia huwezi kuamini hadi leo wapo baadhi ya viongozi ambao hawatambui chochote juu ya ujio wa mkataba huo na ndiyo maana wanashindwa kuusimamia katika ngazi zao,” alisema Bi. Kimaro ambaye ni Mwakilishi wa Watu wenye Ulemavu wa Chama cha Walimu Arumeru.


Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Philipo Meli ambaye ni mwalimu mlemavu (asiyeona) wa Shule ya Sekondari Kimyak wilayani Arumeru amesema Serikali ndiyo inayopaswa kuonesha njia ya kuwajali walemavu hasa katika elimu. Alisema bado nyenzo za kufundishia na kujifunzia kwa watu wenye ulemavu hazipewi kipaumbele jambo ambalo linaweza kuwadidimiza kundi hilo katika harakati ya kujikomboa na hata kujitegemea.


“Mimi ni mwalimu mlemavu wa macho nafundisha kwa kutumia nyenzo maalumu lakini nyenzo hizo sina...kitu cha msingi ambacho Serikali inatakiwa kukikazania kwa kundi hili ni kuwapa elimu kama ilivyo kwa makundi mengine. Binafsi nimetembelea kiwanda cha vitabu pale Dar es Salaam juzi hakuna vitabu kabisa vya walemavu, sasa utamsaidiaje mlemavu kwa mtindo huu...,” alisema Meli akizungumza kijijini Kimyak.


Alisema mara zote anapofuata vitabu kwa ajili ya kufundishia hapati vyote na hata vilivyopo vimepitwa na wakati jambo ambalo ni gumu kuwasaidia watu wenye ulemavu. “Kiwanda hiki ndicho kinachochapisha vitabu kwa watu wenyeulemavu...wanasema hawana vitabu kwa kuwa hawapati ruzuku ya kutosha serikalini, yaani kati ya vitabu 86, ambavyo vinahitajika kwa kada hii ni vitabu sita tu nilipewa nilipofuatilia nyenzo hizo Dar es Salaam, kwa hali hii utamsaidiaje mlemavu.


Aidha alisema elimu ndio nguzo ambayo Serikali inapaswa kuiongezea nguvu kwani iwapo idadi kubwa ya kundi hili litawezeshwa kielimu linaweza kufanya mabadiliko na kujikomboa kiuwezo kabla ya kuingia katika huduma nyingine. 'Habari hii imeandaliwa na mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com) kwa kushirikiana na Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu (ICD) Dar es Salaam'

CHINA KUKABILIANA NA BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO, KUSHIRIKI MAONYESHO MAKUBWA YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM MWAKA JULAI 2012.

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya nchi za nje kutoka Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya watu wa China Bi. Xiao LU (kushoto) akizungumza na wadau wa Biashara kutoka China na Tanzania wakati wa mkutano wa kutangaza maonyesho makubwa ya Bidhaa kutoka nchini China ya mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam.Maonyesho hayo yatafanyika mwezi Julai katika viwanja vya maonyesho vya kimataifa Dar es salaam.

Wadau wa Biashara kutoka China na Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyojili wakati wa mkutano wa kutangaza maonyesho makubwa ya ya mwaka 2012 ya bidhaa kutoka nchini China yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam.
Bw. Lin Zhiyong kutoka China akisalimiana na Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda Tanzania (TCCIA) Bw. Aloys Mwamanga mara baada ya kumalizika kwa mkutanowa kutangaza maonyesho makubwa ya Bidhaa kutoka nchini China ya mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.


CHINA KUKABILIANA NA BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO, KUSHIRIKI MAONYESHO MAKUBWA YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM MWAKA JULAI 2012.


Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara ya nchi hiyo imeandaa maonyesho makubwa ya Afrika ya bidhaa zinazozalishwa na kutengenezwa nchini China kwa lengo la kuinua na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara katika nchi za Afrika.


Akizungumza na wadau wa biashara kutoka China na Tanzania jijini Dar es salaam naibu mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya nchi za nje kutoka Wizara ya Biashara nchini humo Bi. Xiao LU amesema kuwa maonyesho hayo katika nchi za Afrika kwa mwaka huu yatafanyika nchini Tanzania kutokana na uhusiano mzuri wa kibiashara uliopo baina ya China na Tanzania.

Amesema Tanzania ni moja ya eneo muhimu kibiashara katika Afrika Mashariki linalozungukwa na nchi za Ethiopia ,Kenya, msumbiji, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ameongeza kuwa bidhaa za China zinatambulika duniani kote kutokana na upatikanaji wake, bei nzuri na ubora wake huku akifafanua kuwa kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kiteknolojia.


“Hivi sasa bidhaa zetu zinatambulika dunia nzima kutokana na ubora mzuri zilizonao pamoja na bei nzuri,kwa maendeleo makubwa ya teknolojia tuliyonayo tumekuwa tukiongeza ubora wa bidhaa zetu kimataifa” amesema Bi. LU.


Kuhusu maonyesho hayo amesema yatawashirikisha wafanyabishara wakubwa na wadogo yakihusisha bidhaa mbalimbali kutoka China zikiwemo bidhaa za vyakula ,magari,mitambo ya viwandani na kilimo , vifaa vya umeme, vifaa vya mawasiliano, vifaa vya ujenzi pamoja na bidhaa nyingine nyingi yamelenga kuinua na kuimarisha ushirikiano kibiashara kutokana na mabadiliko ya uwekezaji na mabadiliko ya uchumi yanayotokea duniani.


Mbali na bidhaa hizo zitakazoonyweshwa Bi. LU amesema maonyesho hayo yataimarisha ushirikiano wa kiutamadauni baini ya Tanzania na China na nchi nyingine za Afrika ya mashariki.


Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini Tanzania (TCCIA) Bw. Aloys Mwamanga amesema maonyesho hayo ni changamoto kwa wafanyabishara, wakulima na wenye viwanda wa Tanzania kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zao ili waweze kusafirisha bidhaa nyingi zaidi kwenda nchini China na kuongeza pato la Taifa.


Pia ametoa wito kwa washiriki hao kutoka nchini China kujikita katika kuonyesha bidhaa za uzalishaji zinazoweza kuongeza thamani ya mazao zikiwemo bidhaa za kilimo na kuwataka kuongeza juhudi ya upambanaji wa bidhaa zisizokidhi viwango.

UWF YAMTWAA MAMA MJASIRIAMALI ANAYEFUATA NYAYO ZA MWANAMAKUKA 2012!

Pichani shoto ni Meneja matukio na Udhamini wa benki ya NBC,Rachel Remona akimkabidhi Mwanamke Mjasiliamali aliyeibuka na tuzo ya Mwanakuka,Bi.Tatu Mwenda mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita.Pichani kati kulia ni Mwenyekiti wa UWF (waandaji wa tuzo hiyo ya Mwanamakuka),Bi.Mwate Madinda sambamba na Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM,Dina Marios wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa,katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani,iliyofanyika leo,Hafla hiyo imefanyika usiku huu ndani ya hotel ya Serena,jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Pichani shoto ni Meneja matukio na Udhamini wa benki ya NBC,Rachel Remona akimkabidhi mshindi wa pili wa tuzo ya Mwanakuka,Bi. Mwanne Msekalile mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili.Pichani kati kulia ni Mwenyekiti wa UWF (waandaji wa tuzo hiyo ya Mwanamakuka),Bi.Mwate Madinda sambamba na Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM,Dina Marios wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa,katika kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani,iliyofanyika leo,Hafla hiyo imefanyika usiku huu ndani ya hotel ya Serena,jijini Dar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
Meneja matukio na Udhamini wa benki ya NBC,Rachel Remona akimkabidhi mshindi wa tatu wa tuzo ya Mwanakuka,Dada Sikudhani Daudi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja.
Washindi wa tuzo ya Mwanamakuka wakiwa na mdhamini mkuu pamoja na waandaaji wa tuzo hiyo ya Mwanamakuka.
Mshindi wa tuzo ya mwanamke mjasiriamali ya Mwanamakuka,Bi.Tatu Mwenda akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa UWF huku akiwapungia mkono wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Mwenyekiti wa UWF,Bi.Mwate Madinda akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafka hiyo ya tuzo ya Mwanamakuka,kulia kwake ni Meneja Miradi wa UWF,Bi Mariam Shamo.

ORDER ACKNOWLEDGEMENTS FOR THREE ORDERS TUNAHITAJI MICHANGO YENU

                                                     Mama mjamzito akifanyiwa matibabu
Tuna furaha nyingi mbele yenu kutuma maelezo yanayojionesha hapo juu. Tunapenda kutoa tarifa hizi za kujaaliwa kupata mafanikio ya mashine tatu za ultrasound kupitia kampuni maarufu hapa marekani Sonosite Machine hizo Re Manufactured by Sonosite, kama maelezo yalivyoweza Kuonyeshwa katika kiambatanisho hapo chini.
                                               Kujua zaidi huduma ya masine hii Bofya hapa

Kutokana na huduma Hafifu katika sekta ya afya katika hospital zetu machine zote zinakwenda kutumika katika hospital zetu Wete, Machui Clinic na Zanzibar Outreach Program.


Machui Clinics wako tayari kufanya Malipo yao moja kwa moja kupitia sonosite na machine zilizobakia zinatakiwa kulipwa na Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, tunawaomba ndugu wote bila ya kujali itikadi zetu kutoa michango yenu ya hiari katika kusaidia kutuma machine mbili huko Tanzania Zanzibar gharama zimeoneshwa katika attachments shipping pia inatakiwa kufanyika baina seatlle hadi Zanzibar.


Nipo tayari kutoka account yangu kwa wale wote walio tayari kusaidia kutoa michango yao kama ifuatavyo.
Jina: Amin ibrahim ally, Bank of America, Account 32000473, State Washington
Address 13932 NE 14th st apt 8 Bellevue WA 98005
Pay pal account Aminallybts161@live.com


Napenda kumalizia ombi hili kwa kutoa changamoto kwa wazanzibar na watanzania kwa ujumla jukumu la maendeleo ya nchi lipo pia katika mikono yetu siyo serikali pekee tumia nafasi yako kusaidia taifa Lako na wananchi wote na sonosite iko tayari kutizama Matumizi ya Mashine hizi na kutoa missada mengine zaidi hapo baadaye.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na Amin Ibrahim, Number ya simu 425 943-0074. Napenda kutanguliza shurkani zangu za dhati kwenu na pia naomba michango yenu. Ahsanteni.