PICHA ZOTE ZINAONESHA HALI YA AWALI NA ILIVYO SASA BAADA YA MWAKA MMOJA.
Wakati Japan ikiadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea kwa Tsunami na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa rishta 9, wananchi wamepanga kufanya maandamano makubwa kupinga matumizi ya nyuklia. Maandamano hayo yamepangwa kufanyika, sehemu zote nchini Japan, zikiwemo Koriyama eneo uliopo mtambo wa Fukushima Daichi na kusababisha janga kubwa zaidi la kinyuklia kuwahi kushuhudiwa duniani tangu mwaka 1986, ilipotokea ajali ya CHERNOBYL.
Watu zaidi ya 19,000 waliuawa ama kupotea wakati wa janga hilo lililoharibu pia nyumba zaidi ya 370,000. Hadi sasa, waathirika wa ajali hiyo, bado wanaishi katika makazi ya muda huko Iwate, Miyagi na Fukushima.
Mwaka mmoja baada ya ajali hiyo kutokea kwenye kinu cha nyuklia cha Fukushima nchini Japan, swali linalozuka ni je, umeme unaohitajiwa na nchi hiyo iliyostawi kiviwanda utatoka wapi kwa siku zijazo?
Inashangaza kuona kwamba nchini Japan kila kitu kinakwenda sawa licha ya kwamba sehemu ndogo tu ya umeme wa nguvu ya nyuklia iliyokuwa inatumika zamani ndio inayotumika hivi sasa.
Baada ya janaga hilo, hakuna aliyefikiri kwamba Japan nchi ya tatu kwa utajiri duniani, ingeweza kujimudu bila ya kuwa na umeme utokanao na nguvu ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment