Sunday, March 11, 2012

CHINA KUKABILIANA NA BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO, KUSHIRIKI MAONYESHO MAKUBWA YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM MWAKA JULAI 2012.

Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya nchi za nje kutoka Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya watu wa China Bi. Xiao LU (kushoto) akizungumza na wadau wa Biashara kutoka China na Tanzania wakati wa mkutano wa kutangaza maonyesho makubwa ya Bidhaa kutoka nchini China ya mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam.Maonyesho hayo yatafanyika mwezi Julai katika viwanja vya maonyesho vya kimataifa Dar es salaam.

Wadau wa Biashara kutoka China na Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyojili wakati wa mkutano wa kutangaza maonyesho makubwa ya ya mwaka 2012 ya bidhaa kutoka nchini China yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam.
Bw. Lin Zhiyong kutoka China akisalimiana na Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda Tanzania (TCCIA) Bw. Aloys Mwamanga mara baada ya kumalizika kwa mkutanowa kutangaza maonyesho makubwa ya Bidhaa kutoka nchini China ya mwaka 2012 yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Watu wa China jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.


CHINA KUKABILIANA NA BIDHAA ZISIZOKIDHI VIWANGO, KUSHIRIKI MAONYESHO MAKUBWA YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM MWAKA JULAI 2012.


Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara ya nchi hiyo imeandaa maonyesho makubwa ya Afrika ya bidhaa zinazozalishwa na kutengenezwa nchini China kwa lengo la kuinua na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara katika nchi za Afrika.


Akizungumza na wadau wa biashara kutoka China na Tanzania jijini Dar es salaam naibu mkurugenzi wa Idara ya Biashara ya nchi za nje kutoka Wizara ya Biashara nchini humo Bi. Xiao LU amesema kuwa maonyesho hayo katika nchi za Afrika kwa mwaka huu yatafanyika nchini Tanzania kutokana na uhusiano mzuri wa kibiashara uliopo baina ya China na Tanzania.

Amesema Tanzania ni moja ya eneo muhimu kibiashara katika Afrika Mashariki linalozungukwa na nchi za Ethiopia ,Kenya, msumbiji, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ameongeza kuwa bidhaa za China zinatambulika duniani kote kutokana na upatikanaji wake, bei nzuri na ubora wake huku akifafanua kuwa kuwa nchi hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kiteknolojia.


“Hivi sasa bidhaa zetu zinatambulika dunia nzima kutokana na ubora mzuri zilizonao pamoja na bei nzuri,kwa maendeleo makubwa ya teknolojia tuliyonayo tumekuwa tukiongeza ubora wa bidhaa zetu kimataifa” amesema Bi. LU.


Kuhusu maonyesho hayo amesema yatawashirikisha wafanyabishara wakubwa na wadogo yakihusisha bidhaa mbalimbali kutoka China zikiwemo bidhaa za vyakula ,magari,mitambo ya viwandani na kilimo , vifaa vya umeme, vifaa vya mawasiliano, vifaa vya ujenzi pamoja na bidhaa nyingine nyingi yamelenga kuinua na kuimarisha ushirikiano kibiashara kutokana na mabadiliko ya uwekezaji na mabadiliko ya uchumi yanayotokea duniani.


Mbali na bidhaa hizo zitakazoonyweshwa Bi. LU amesema maonyesho hayo yataimarisha ushirikiano wa kiutamadauni baini ya Tanzania na China na nchi nyingine za Afrika ya mashariki.


Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini Tanzania (TCCIA) Bw. Aloys Mwamanga amesema maonyesho hayo ni changamoto kwa wafanyabishara, wakulima na wenye viwanda wa Tanzania kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zao ili waweze kusafirisha bidhaa nyingi zaidi kwenda nchini China na kuongeza pato la Taifa.


Pia ametoa wito kwa washiriki hao kutoka nchini China kujikita katika kuonyesha bidhaa za uzalishaji zinazoweza kuongeza thamani ya mazao zikiwemo bidhaa za kilimo na kuwataka kuongeza juhudi ya upambanaji wa bidhaa zisizokidhi viwango.

No comments:

Post a Comment