su1: Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Marehemu Jeremiah Sumari likiwasili katika uwanja wa Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo January 21, 2012 tayari kwa kupewa heshma za mwisho.
Rais Kikwete akitoa heshima zake za mwisho.
Rais Kikwete akimpa pole mjane Mama Miriam Sumari.
Rais Kikwete akiongoza umati mkubwa wa waombolezaji katika halfa hiyo.
Rais Kikwete, Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman, Spika Anne Makinda na kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe kwenye hafla hiyo...PICHA NA IKULU.
Sunday, January 22, 2012
MAIGE ATAKA VIGOGO WALIOVAMIA MISITU WATOLEWE!
Na Tulizo Kilaga, Ruvu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige, amewaagiza watendaji wa misiti kuhakikisha wanafanya zoezi la kitaifa la kuhakiki mipaka ya misitu nchini na kuwatoa wavamizi wote waliopo ndani ya hifadhi za misitu.
Mhe. Maige aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa katika ziara ya kutembelea Msitu wa Hifadhi wa Ruvu Kaskazini uliopo Kibaha, mkoani Pwani baada ya kuelezwa kuwa kuna baadhi ya vigogo wameuziwa na wanakijiji maeneo makubwa yaliopo ndani ya hifadhi kwa kujua ama kutokujua na kuweka mawe ya ardhi hali inayowawia vigumu kuwatoa. Kufuatia taarifa hiyo, Mhe. Maige aliwaagiza watendaji wake kuhakikisha wanashirikiana na wataalamu wa ramani kutoka Wizara ya Ardhi kuhakiki mipaka ya misitu na kuwabomolea wale wote walioko ndani ya mipaka ya hifadhi.
“Hakikini mipaka yenu na baada ya kubainisha mipaka hiyo, kama ambavyo tunavyofanya kule kwingine, kitakachofuata kwa wale walioko ndani ya hifadhi, kuna ile mikasi mwekundu, bomoa, wabomolewe haraka iwezekanavyo na hapo ndipo tutakapowabaini wazito ama wanene waliovamia hifadhi,” alisema Mhe. Maige.
Aidha, aliongeza kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kwa kufanya uchunguzi kwani kuna maeneo ambayo wataalamu wa misitu waliopewa dhamana ya kuyalinda kwa makusudi wanajidahi hawajui mipaka na kuruhusu ardhi imegwe.
“Kuna matukio mawili matatu ambayo afisa misitu ameandikiwa na afisa ardhi, tunataka kutoa eneo hili kwa muwekezaji fulani, tunaomba utuhakikishie mipaka ya hifadhi kwamba haifiki kwenye eneo hilo, akaandika nakuhakikishia eneo hilo liko nje kwa sababu tu ameshawishiwa kwa namna ambayo ni vigumu mimi na wewe kujua,” “Sasa nitakapobaini watu wa namna hiyo ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wameridhia shughuli za uendelezaji ama utoaji wa hati ifanywe, hao nitashughulika nao,” alisema Mhe. Maige.
Aliongeza kuwa hivi sasa kuna matapeli wa ardhi hasa viongozi wa vijiji ambao pindi wanapoombwa ardhi na wawekezaji, huwapimia ardhi hata ile iliyoko ndani ya pori tengefu kwa kisingizio kuwa hawajui mipaka ya vijiji vyao. Anasema kuwa viongozi kujifanya hawajui mipaka ni utapeli, hivyo pale itakapotokea watu waliouziwa maeneo na viongozi hao na kubomolewa, viongozi wa vijiji watawajibika kuwarudishia gharama zao kama si kuwatafutia ardhi mbadala kwenye maeneo ya vijiji vyao.
Mhe. Maige alisema kuwa kwa uharaka wa tatizo hilo la uvamizi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Bi. Monica Kagya ahakikishe kuwa tathimini inafanyika na fedha zinapatikana kwa ajili ya kuweka bikoni angalau kila baada ya mita 500 ili kutatua tatizo. Akielezea tatizo hilo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS alisema wakala wake uko mbioni kuajiri askari wa misitu watakaokuwa na jukumu la kuilinda misitu yote nchini ili kuondoa tatizo la uvamizi.
“Hivi sasa tuko katika mchakato wa kumalizia mpango kazi wa TFS na mara baada ya kumalizika tutatoa ajira kwa askari misitu ambao jukumu lao kuu litakuwa ni kuhakikisha misitu yetu haivamiwi. Hili litakuwa suluhisho la tatizo tulilonalo hivi sasa kwani muda wote misitu italindwa kama zinavyolindwa mashine za pesa,” alisema Bi. Kagya.

KOZI YA YA KIMATAIFA YA KUFUNDISHA MCHEZO WA NGUMI YAENDELEA!
Kozi ya Makocha wa Ngumi inayoendelea Kibaha, Pwani katika shule ya Filbart Bayi, inaendelea vema chini ya mkufunzi aliyeletwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Josef Diouf kutoka Senegal.
Ikiwa imefika siku ya sita makocha wanaohudhuria mafunzo hayo ya siku kumi, wamelizika na kiwango cha mkufunzi huyo kwa kusema kuwa mbinu za kiufundi na ujanja wa ufundishaji wa mchezo wa ngumi anazo wafundisha ni za kisasa na kwamba kwa sasa wameelewa msingi wa ufundishaji,hasa kwa kumwanzisha, kumwendeleza mchezaji hadi kufikia kuwa mchezaji wa kimataifa toufauti na awali ambapo walikuwa wanafundisha kwa mazoea bila kuwa na mbinu za kuwafanya wachezaji ili kuleta upinzani hasa katika mashindano ya kimataifa.
Lakini pia wamejifunza namna ya kuandaa ratiba za ufundishaji za siku kwa siku ,wiki,mwezi na ratiba ya mashindano yanayowakabili
Kwa kujigamba Makocha kutoka mikoani wamesema ujuzi wao wataanza kuonyesha katika mashindano ya Taifa yatakayofanyika katikati ya mwezi wa February ya kuwa kutakuwa na ushindani mkali sana hasa kwa kuzingatia mikoa mingi makocha wake wamepata mafunzo hayo,na sasa timu za vyombo vya ulinzi na usalama na zile za Dar es salaam ziwe tayari kupata upinzani wa hali ya juu kwa kuwa sasa hata vilabu vya kutoka mikoani pia zina mbinu na ujanja wa ufundishaji kulingana na mabadiliko ya mchezo wa Ngumi Duniani.
Kozi hiyo inatazamiwa kumalizika tarehe 24/01/2012 na walimu watakaokuwa wamefaulu watatunukiwa vyeti vya kimataifa vya daraja la kwanza(level 1) na kuingizwa katika Database za Chama cha Ngumi cha Dunia AIBA na kwamba watakuwana haki ya kufundisha mchezo wa Ngumi popote Duniani. Wakati huo BFT kwa masikitiko makubwa inasikitika kupatwa na msiba wa bondia wa timu ya Taifa Godfrey Mbunda aliyefariki kwa kugongwa na gari wakati yeye akiwa anaendesha pikipiki maeneo ya mbezi.ni pigo kubwa katika medani ya mchezo wa ngumi kwa kuwa bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa suala la maendeleo ya mchezo wa ngumi Tanzania
Makore Mashaga
KATIBU MKUU.

VODACOM M-PESA GOES ANOTHER MILE!
• Its customers with CRDB accounts to access accounts via mobile phone
Vodacom customers with accounts with CRDB Bank are now able to keep or to move money from their accounts to their mobile phones via Vodacom M-Pesa service. The move to launch this service brings a solution towards a serious challenges faced by Bank customers such as standing on a long queue and travelling long distance to visit their bank branches to be able to access their accounts for depositing and withdrawing.
The introduction of the service will make the process of customers withdrawing and depositing money to their account at CRDB bank easy through mobile phone anywhere in the country and at any time without physical contact with bank. “This initiative came very timely and that we are very optimistic that the problems of standing on queue neither travelling will be no longer for a M-PESA customers who are also CRDB customers since principal transactions of bank – withdrawal and depositing can be done via a mobile phone.” Said Vodacom Managing Director Mr. Rene Meza.
“Using M-PESA agents network scattered every corner of the country, Vodacom Tanzania a leading mobile phone telecommunications firm in the country proves its commitment of bringing innovative services in the market that really connect and changing people’s lives through mobile phone technologies” He added. Emphasizing on this, Mr. Meza said the service is for all Vodacom customers who have CRDB accounts, regardless to their account status. “This service is for all Tanzanians who have CRDB accounts and are Vodacom customers and registered with M-PESA service”. He said.
This is another first from Vodacom, partnership with CRDB will bring banking services on finger tips of mobile phone users and save M-PESA customers of their valuable time to attend to other activities.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MRADI WA MAJI WA CHIUMBATI NACHINGWEA, APOKEA KADI YA MWENYEKITI WA CHADEMA (W) NACHINGWEA!
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye eneo la mradi wa maji wa Chiumbati Miembeni, wakati alipotembelea mradi huo wa Nachingwea Masasi, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi, jana Januari 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa maji wa Chiumbati, Francis Fumbuka, wakati alipotembelea mradi huo unaoendelea na ujenzi Nachingwe akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi, iliyoanza jana Januari 20, 2012. Kushoto ni mkewe, Mama Zakhia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kadi ya uanachama kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, Hassan Mkope, aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na CCM, wakati Makamu alipotembelea mradi wa maji wa Chiumbati Nachingwea, akiwa katika zaiara yake ya mkoa wa Lindi, jana januari 20, 2012.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Profesa Mtopea, akizungumza kutoa shukrani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Nachingwea, wakati alipokuwa akiondoka katika mradi wa maji wa Chiumbati jana, januari 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Nachingwea, wakati alipokuwa akiondoka katika mradi wa maji wa Chiumbati jana, januari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YAKE MKOA WA LINDI, AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUZINDUA MAJENGO YA SHULE YA WASICHANA NACHINGWEA!
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Nachingwea, wakati wa ziara yake Mkoa wa Lindi iliyoanza leo Januari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AANZA ZIARA YA
KISERIKALI MKOANI LINDI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameanza ziara ya siku nne ya kiserikali mkoani Lindi leo Ijumaa Januari 20, 2012. Katika ziara hii Makamu wa Rais anatembelea wilaya za Nachingwea, Lindi na Kilwa. Hii ni mara ya kwanza kwa Dkt. Bilal kufanya ziara mkoani hapa akiwa Makamu wa Rais ambapo anapata fursa ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kujiendeleza katika kazi zao mbalimbali.
“Nimefarijika sana kuwa katika mkoa huu, nimepokea mapokezi mazuri na nimefarijika sana kuna wananchi wa mkoa wa Lindi namna wanavyojitutumua katika kusaka maendeleo ya maisha yao,”alisema Dkt. Bilal siku ya kwanza ya ziara yake wakati akihutubia wananchi wa Chiumbali ambapo hapo kuna mradi mkubwa wa maji unatoka Masasi na unaolenga kutoa maji kwa wilaya za Masasi Nachingwea, mradi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ukosefu wa maji katika Wilaya ya Nachingwea hasa nyakati za
kiangazi.
Kwa sasa wilaya ya Nachingwea iko katika hatua za kutanua kilimo na hali ya hewa wilayani hapa katika kipindi hiki inaonyesha kuwa upo uwezekano wa wilaya hii kupata mavuno mazuri ya mahindi ambayo yanaonyesha kustawi huku ardhi ya wilaya hii ikiwa na uwezo wa kumudu kuwa na mazao yenye rutuba bila kutumia mbolea za viwandani. Makamu wa Rais pia amekuwa katika shughuli za kuhamasisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi hasa katika shule ya Nachingwea ambayo ni maalum kwa wanafunzi wa kike ambayo imeanzishwa mwaka huu na ina wanafunzi 50. Shule hii ina dhamira ya kuwa na michepuo ya sayansi na imejengwa kwa lengo la kukabiliana na tatizo la mimba kwa watoto sambamba na ndoa za utotoni.
Mkoa wa Lindi unakabiliwa na changamoto nyingi na moja kubwa ni soko la zao la Korosho ambapo sasa wakulima wana shauku kubwa ya kupata malipo yao ya pili kufuatia mfumo wa stakabadhi ghalani, malipo ambayo hayajatolewa.Katika kukabiliana na tatizo hili Makamu wa Rais amemwagiza Waziri mwenye dhamana ya Kilimo na Ushirika kukutana na wadau wa zao la Korosho ili kujadiliana na kutoa jibu la tatizo hili katika kipindi kifupi kijacho, ili kuwapa wananchi hamasa ya kuendelea kuzalisha korosho.
Makamu wa Rais pia anasisitiza juu ya wananchi kutumia demokrasia iliyopo nchini kwa kukosoa serikali huku wakibaini kuwa, demokrasia ina mipaka yake na kwamba wajadiliane kwa busara katika mijadala ya kutafuta Katibampya na mwisho watambue hawana eneo jingine duniani linalowathamini zaidi
ya Tanzania.

NAPE AWA MGENI RASMI SHULE YA NSUMBI, MWANZA ALIKOSOMEA!
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo Busagi, katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Jumla ya wahitimu 374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Tifugundulwa Tumbika katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Tumbika alikabidhiwa cheti hicho kwa kuibuka mwanafunzi bora katika kuzungumza Kiingereza. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari ya Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane na kumi) Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo. Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika shule hiyo hadi kidato cha nne mwaka ambako alimaliza mwaka 97. Watatu ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.(Picha zote na Bashir Nkoromo).
NA MWANDISHI WETU, MWANZA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwake, kukarabati vyumba na kuweka nyavu za mbu nwenye madirisha katika mabweni ya shule ya sekondari ya wavulana ya Nsumba, jijini Mwanza.
Akizungumza na mamia ya wanafunzi, walimu, walezi na wazazi kwenye mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo, Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kazi hiyo itafanayika kwa CCM kushirikiana na marafiki zake.
Nape alisema, kwa kushirikisha marafiki hao wa CCM, pia Chama kitaitafutia shule hiyo gari kwa ajili ya usafiri na huduma nyingine muhimu kwa za shule.Alisema mbali na misaada hiyo CCM itaisaidia pia shule hiyo kompyuta si chini ya tano na viti na meza kwa ajili ya kulia chakula.
Nape alitoa ahadi hizo kujibu maombi yaliyotolewa na risala iliyosomwa na wanafunzi wa kidato cha sita muda mfupi kabla ya kuwakabidhi vyeti.Kuhusu vifaa vya maabara Nape aliahidi kulifikishia suala hilo serikali ili ione namna ya kuisaidia shule hiyo ambapo yeye binafsi kama shukrani ya kusoma Nsumba, atamwaga vifaa vya michezo.
Nape aliyehitimu kidato cha nne mwaka 1997 Nsumba, aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo waendelee kuwatia moyo watoto wao na kuwasaidia kwa hali na mali ili wafikie matarajio yao kielimu na kuifanya iwe mfano wa kuigwa wa kutoa viongozi bora wa umma. Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 374 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu kidato cha sita.

BIBI MALAIKA ASHEREKEA KUFIKISHA MIAKA 75!
Dada Cosmaya (wa pili kulia mwenye nguo nyeupe) akiwa na wifi yake Mama wa mitindo Asia Khamsin pamoja na marafiki zao wengine waliohudhurua katika maadhimisho ya miaka 75 kuzaliwa kwa mama yake mzazi Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mama wa mitindo Asia Khamsin akiwa na shemeji yake ambaye ni mtoto wa mwisho wa Bi. Malaika wakiwa katika maadhimisho ya miaka 75 ya kuzaliwa kwa mama yake mzazi Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika akifurahia na kushangiliwa na marafiki, watoto na wajukuu zake kwa kutimiza miaka 75 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Bibi Malaika (katikati) ambaye amefikisha miaka 75 akiwa na mwanae mama Khatibu pamoja na mke wa mwanae Mama wa mitindo Asia Khamsin.
Bibi Malaika akisalimia na Balozi mstaafu wa Ufaransa Mhando katika sherehe ya kumpongeza Bibi Malaika kufikisha miaka 75.

KUMBE INADAIWA MCHUMBA WAKE DK SLAA NDIYE ALIYEMZUIA KUSALIMIA NA JK!
Mazishi ya Mbunge wa Chadema, Mheshimiwa Regia Mtema yamethibitisha kuwa vituko na vioja vya Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa Wilbroad Slaa na “mchumba wake,” Josephine Mushumbusi havijaisha hata kama sasa wanaishi pamoja.
Kwa namna ambayo sasa imethibisha nani hasa mwenye madaraka, mamlaka na kauli ndani ya nyumba yao, Josephine Mushumbusi amemzuia “mchumba/mume” kwenda kumpa mkono Kiongozi wa nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mara baada ya Rais Kikwete kuingia katika makaburi ya familia ya Mtema mjini Ifakara kiasi cha saa tisa unusu mchana, Mheshimiwa Slaa ambaye alikuwa amekaa peke yake na Josephine pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema, alionyesha ishara ya kwenda kumsalimia Mheshimiwa Rais Kikwete ambaye alikuwa jukwaa kuu.
Lakini Josephine Mushumbusi alimzuia mchumba wake asiende kumsalimia Rais Kikwete akimwambia, “usiende…italeta maneno ya bure.” Kwa namna inayothibitisha nani bosi ndani ya nyumba, Mheshimiwa Slaa alijikunja na kusalimu amri akisema, “haya bwana”.
Kila dalili za tukio hilo zimethibisha kuwa ubabe na ushujaa ambao Mheshimiwa Slaa huonyesha hadharani kwa kutukana, kukejeli na kuwashambulia wenzake katika siasa akiwamo Rais Kikwete ni nguvu za soda tu zisizotamba mbele ya Josephine ambaye alionyesha udhitibi na umwamba wake hadharani leo.Lakini tukio la leo pia limethibitisha kwa mara nyingine kiwango cha kinyogo ambacho familia ya Slaa na mchumba wake wanayo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete tokea Rais alipowabwaga na kumsambaratisha kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, 2010.
Tokea wakati huo, Mheshimiwa Slaa hajapata kumsema vizuri Rais Kikwete, hajapata hata kumtambua hadharani pamoja na kujua kuwa alishindwa kihalali, hajapata kumsalimia wala kumpa Kiongozi huyo wa nchi mkono hadharani hata fursa inapojitokeza kama leo. Kwa ufupi, tukio la leo na mengine mengi yalimtangulia limethibitisha kuwa Mheshimiwa Slaa ni kiongozi mwenye kinyongo na asiyekuwa na heshima kabisa.
Kama ambavyo wamepata kusema wengine hana sifa za kuwa na kiongozi mkuu wa nchi yetu hii inayoongozwa kwa misingi ya maelewano na siyo kwa misingi ya chuki ambazo anazionyesha Mheshimiwa Slaa. Kwa hili Dr. Slaa Kachemsha, kadhihirisha wazi kuwa hana siyo tu ukomavu wa uongozi bali pia ukomavu wa kisiasa. Sasa naelewa pia kwa nini Slaa upadre ulimshinda. Ni jambo la ajabu kuwa mfiwa kama alivyokuwa Slaa leo kwa sababu yeye amempoteza Mbunge anakataa vipi kwenda kumsalimia mwombolezaji ambaye amekwenda kumpa pole na kumjulia hali. Huu ni ubinadamu na uungwana kweli?
Mzee Slaa anashindwa na wadogo zake kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambao walipeana mikono na kukaa pamoja na Mheshimiwa Rais, kubadilishana mawazo na kuomboleza kwa pamoja.
Subscribe to:
Posts (Atom)