Sunday, January 22, 2012

NAPE AWA MGENI RASMI SHULE YA NSUMBI, MWANZA ALIKOSOMEA!

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo Busagi, katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Jumla ya wahitimu 374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeyo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Tifugundulwa Tumbika katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, Mwanza. Tumbika alikabidhiwa cheti hicho kwa kuibuka mwanafunzi bora katika kuzungumza Kiingereza. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma shule ya sekondari ya Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane na kumi) Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo. Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika shule hiyo hadi kidato cha nne mwaka ambako alimaliza mwaka 97. Watatu ni Mkuu wa shule hiyo Josephat Zakeo.(Picha zote na Bashir Nkoromo).

NA MWANDISHI WETU, MWANZA



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwake, kukarabati vyumba na kuweka nyavu za mbu nwenye madirisha katika mabweni ya shule ya sekondari ya wavulana ya Nsumba, jijini Mwanza.
Akizungumza na mamia ya wanafunzi, walimu, walezi na wazazi kwenye mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo, Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kazi hiyo itafanayika kwa CCM kushirikiana na marafiki zake.


Nape alisema, kwa kushirikisha marafiki hao wa CCM, pia Chama kitaitafutia shule hiyo gari kwa ajili ya usafiri na huduma nyingine muhimu kwa za shule.Alisema mbali na misaada hiyo CCM itaisaidia pia shule hiyo kompyuta si chini ya tano na viti na meza kwa ajili ya kulia chakula.


Nape alitoa ahadi hizo kujibu maombi yaliyotolewa na risala iliyosomwa na wanafunzi wa kidato cha sita muda mfupi kabla ya kuwakabidhi vyeti.Kuhusu vifaa vya maabara Nape aliahidi kulifikishia suala hilo serikali ili ione namna ya kuisaidia shule hiyo ambapo yeye binafsi kama shukrani ya kusoma Nsumba, atamwaga vifaa vya michezo.

Nape aliyehitimu kidato cha nne mwaka 1997 Nsumba, aliwataka wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo waendelee kuwatia moyo watoto wao na kuwasaidia kwa hali na mali ili wafikie matarajio yao kielimu na kuifanya iwe mfano wa kuigwa wa kutoa viongozi bora wa umma. Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 374 walitunukiwa vyeti vya kuhitimu kidato cha sita.

No comments:

Post a Comment