Sunday, January 22, 2012
KUMBE INADAIWA MCHUMBA WAKE DK SLAA NDIYE ALIYEMZUIA KUSALIMIA NA JK!
Mazishi ya Mbunge wa Chadema, Mheshimiwa Regia Mtema yamethibitisha kuwa vituko na vioja vya Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa Wilbroad Slaa na “mchumba wake,” Josephine Mushumbusi havijaisha hata kama sasa wanaishi pamoja.
Kwa namna ambayo sasa imethibisha nani hasa mwenye madaraka, mamlaka na kauli ndani ya nyumba yao, Josephine Mushumbusi amemzuia “mchumba/mume” kwenda kumpa mkono Kiongozi wa nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mara baada ya Rais Kikwete kuingia katika makaburi ya familia ya Mtema mjini Ifakara kiasi cha saa tisa unusu mchana, Mheshimiwa Slaa ambaye alikuwa amekaa peke yake na Josephine pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema, alionyesha ishara ya kwenda kumsalimia Mheshimiwa Rais Kikwete ambaye alikuwa jukwaa kuu.
Lakini Josephine Mushumbusi alimzuia mchumba wake asiende kumsalimia Rais Kikwete akimwambia, “usiende…italeta maneno ya bure.” Kwa namna inayothibitisha nani bosi ndani ya nyumba, Mheshimiwa Slaa alijikunja na kusalimu amri akisema, “haya bwana”.
Kila dalili za tukio hilo zimethibisha kuwa ubabe na ushujaa ambao Mheshimiwa Slaa huonyesha hadharani kwa kutukana, kukejeli na kuwashambulia wenzake katika siasa akiwamo Rais Kikwete ni nguvu za soda tu zisizotamba mbele ya Josephine ambaye alionyesha udhitibi na umwamba wake hadharani leo.Lakini tukio la leo pia limethibitisha kwa mara nyingine kiwango cha kinyogo ambacho familia ya Slaa na mchumba wake wanayo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete tokea Rais alipowabwaga na kumsambaratisha kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, 2010.
Tokea wakati huo, Mheshimiwa Slaa hajapata kumsema vizuri Rais Kikwete, hajapata hata kumtambua hadharani pamoja na kujua kuwa alishindwa kihalali, hajapata kumsalimia wala kumpa Kiongozi huyo wa nchi mkono hadharani hata fursa inapojitokeza kama leo. Kwa ufupi, tukio la leo na mengine mengi yalimtangulia limethibitisha kuwa Mheshimiwa Slaa ni kiongozi mwenye kinyongo na asiyekuwa na heshima kabisa.
Kama ambavyo wamepata kusema wengine hana sifa za kuwa na kiongozi mkuu wa nchi yetu hii inayoongozwa kwa misingi ya maelewano na siyo kwa misingi ya chuki ambazo anazionyesha Mheshimiwa Slaa. Kwa hili Dr. Slaa Kachemsha, kadhihirisha wazi kuwa hana siyo tu ukomavu wa uongozi bali pia ukomavu wa kisiasa. Sasa naelewa pia kwa nini Slaa upadre ulimshinda. Ni jambo la ajabu kuwa mfiwa kama alivyokuwa Slaa leo kwa sababu yeye amempoteza Mbunge anakataa vipi kwenda kumsalimia mwombolezaji ambaye amekwenda kumpa pole na kumjulia hali. Huu ni ubinadamu na uungwana kweli?
Mzee Slaa anashindwa na wadogo zake kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambao walipeana mikono na kukaa pamoja na Mheshimiwa Rais, kubadilishana mawazo na kuomboleza kwa pamoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment