Wednesday, September 7, 2011

HOSPTALI YA AMANA YAKABILIWA NA TATIZO LA MAJI SAFI NA SALAMA!

Hospitali ya Amana iliyoko jijini DSM imetajwa kwamba inakabiliwa na tatizo la maji linalosababishwa na uchakavu wa mabomba ya maji safi na maji taka hali ambayo inaathiri ufanisi wa usafi pamoja na shughuli za upasuaji kushindwa kufanyika kwa wakati hospitalini hapo.

Mkurugenzi wa kampuni ya SHEAR ILLUSION Bi SHEKHA NASSER amesema kufuatia hali hiyo wameamua kufanya tafrija ya hisani ya kuchangisha jumla ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kukarababti na kuimarisha mifumo ya maji safi na maji taka katika hospitali hiyo pamoja na kuwasaidia wanawake walioathirika na ugonjwa wa fistula katika hospitali ya CCBRT.


Nae Mkurugenzi wa Hospitali ya Amana Dokta MESHACK SHIMWELA amekiri kuwa shughuli mbalimbali katika hospitali hiyo zikiwemo za usafi na upasuaji zinakwama kufanyika kutokana na kukosekana kwa maji hivyo endapo mfumo wa maji ukiimarishwa , hospitali itaweza kutoa huduma bora na salama kwa wagonjwa na wafanyakzi na kudhibiti maambukizi. Tafrija hiyo ya hisani inatarajia kufanyika Octoba mosi mwaka huu jijini DSM.

No comments:

Post a Comment