Saturday, March 17, 2012

WANAFUNZI WA UDOM WAFANYA ZIARA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA VIWANDANI ILIYOPO DODOMA MJINI NA KUKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA USAFI LEO!

Mmoja wa Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akishusha Baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi wakati wanafunzi wa UDOM walipowasili Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo Manispaa ya Dodoma Mjini mchana wa leo.
Mwanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Areman Kaziguto (mwenye fulana nyeupe) akitoa maelezo machache mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya viwandani iliyopo manispaa ya Dodoma mjini ambapo wanafunzi wa UDOM leo walifanya ziara na kukabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia Usafi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Viwandani ambao ni wanachama wa klabu ya mazingira shule hapo wakiwa makini kusikiliza somo lililotolewa juu ya umuhimu wa kutunza mazingira mchana wa leo.
Picha hapo juu ni Mwanafunzi wa UDOM Josephat Lukaza akitoa Maelezo jinsi ya matumizi sahihi ya vifaa vya kufanyia na kutunzia uchafu kwa wanafunzi wa klabu ya mazingira ya shule ya sekondari ya viwandani iliyopo Dodoma mjini.
Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo mjini Dodoma wakisikiliza kwa makini baadhi ya maelezo kutoka Kwa Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mchana wa leo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa makini kusikiliza Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira Wakichangia Mada mbalimbali kuhusu Umuhimu wa Kutunza mazingira wakati walipotembelewa na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo mchana.
Mwenyekiti Wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani Idrisa Ramadhani akitoa shukrani kwa wanafunzi wa UDOM waliotembelea shuleni hapo na kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi
Mwalimu wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani Bi Ester Bahati akitoa shukrani za dhati kwa wanafunzi wa UDOM waliotembelea Shule hiyo na Kutoa Misaada ya Vifaa vya Kufanyia Usafi leo Mchana.
Wanafunzi wa Klabu ya Mazingira ya Shule ya Sekondari ya Viwandani iliyopo kwenye manispaa ya Dodoma wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) waliotembelea Shule hiyo Mchana wa leo.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog - http://josephatlukaza.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment