Wananchi wa kijiji cha Ngabobo wakimthibitishia mratibu wa kampenbi za CCM uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba (kshoto) kuwa watampa kura mgombea wa CCM Sioi Sumari , wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho, jana.
Mwigulu (kushoto) akiwa amejichanganya na wamasai kwenye mkutano wa Ngabobo, Ngarenanyuki wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho juzi.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wasira akimnadi Sioi mkutano wa Uwiro, Ngarenanyuki.
Mkazi wa Kijiji cha Uwiro kata ya Ngarenanyuki, jimbo la Arumeru Mashariki, Elielisia Kaayao akibandika kwenye duka lake bango la mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Sioi Sumari, jana.
Wazee na Kijana wakimsikiliza kwa makini mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jana kijiji cha Uwiro, kata ya Ngarenanyuka.
Sioi na Mbunge wa Ngorongoro, Lekule Laiza wakizungumza jambo baada ya mkutano wa kampeni wa kijiji cha Uwiro, Ngarenanyuki. kulia ni Wasira.
CCM naifagilia ki kweli kweli kabisa na watakia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huu hakuna matatizoo Mhe Mwigulu na team yako kazeni buti, wana CCM wooote Tanzania nzima tuko nyuma yenu na ushindi kwa CCM ni lazima kwa CCM,
ReplyDelete