Tuesday, March 20, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) KITAIFA MKOANI TANGA

Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto) wa Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa Deogratias Kessy wa banda la VETA Moshi, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA mkoa wa Tanga, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Tangamano, Kwa ajili ya kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na mwasisi wa Chuo cha Gemmologiacal and jewelry Vocation cha Arusha, Peter Salla, kuhusu matumizi yam awe ya madini, wakati akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
6 na7:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Machi 19 Kitaifa mkoani Tanga. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments:

Post a Comment