Rais JAKAYA KIKWETE amekiri kuwa serikali imekuwa ikitumia shilingi bilioni 700 kwa mwaka kupeleka wagonjwa wa moyo nchini India huku asilimia 60 ya wagonjwa ambao wamekuwa wakipelekwa nchini humo kwa ajili ya kupata matibabu ni wale wenye matatizo ya moyo.
Rais KIKWETE ameyasema hayo hii leo wakati wa mkutano wa kimataifa wa madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo uliofanyika jijini DSM.
Kwa upande wake Katinbu Mkuu waWizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi BLANDINA NYONI amesema Serikali inao mkakati mkubwa katika kukabiliana na uhaba wa Madaktari bingwa wa Moyo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya Wabafunzi wanaoingia kwenye vyuo vya unesi watekinolojia na wafamasia.
No comments:
Post a Comment