Tuesday, December 6, 2011

WANAFUNZI MTAKATIFU JOHN BUGURUNI KWA MALAPA WAANDAMA HADI BODI YA MIKOPO KUDAI FEDHA ZAO!

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu JOHN kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam wameandamana hadi Ofisi za Bodi ya Mikopo wakilalamika kutopatiwa pesa zao za mikopo tangu walipofungua chuo mapema Oktoba mwaka huu.



Wakizungumza jijini Dar es Salaam, wanafunzi hao wamesema pamoja na kufika katika ofisi hizo kutoa malalamiko yao, uongozi wa bodi hiyo haukutoa ushirikiano unaotakiwa. Clouds Fm ilipotaka kupata ufafanuzi wa madai hayo, uongozi wa bodi ya mikopo haukuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

No comments:

Post a Comment