Baada ya Uongozi wa Soko la Feri, Jijini Dar es salaam kueleza kutoridhishwa kwake na maamuzi yaliyofikiwa na Uongozi wa Manispaa ya Ilala wa kumtafuta Mkandarasi wa kukusanya mapato katika Soko hilo bila kuwashirikisha hii leo Uongozi wa Manispaa hiyo umeyatolea ufafanuzi zaidi madai hayo.
Akizungumza na kituo hiki, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bwana JOHN WANGA, amesema kuwa zoezi la kumtafuta mkandarasi huyo lilifanyika kwa uwazi huku Uongozi wa Soko hilo ukishirikishwa katika mchakato huo.
No comments:
Post a Comment