Tuesday, December 6, 2011

BREAKING NEEEEEEEEEEWS! ZAIDI WATU 10 WAFARIKI KIMARA KOROGWE BAADA YA AJALI YA LORI LA NG'OMBE NA HIACE!

Breaking News!



Habari zilizotufikia hivi punde chumba cha habari zinasema kuwa zaidi ya watu 10 wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kimara Korogwe na kuhusisha lori lililobeba ng’ombe likitokea mwelekeo wa Morogoro na basi dogo la abiria.


Hadi sasa imedaiwa kuwa askari wa usalama barabarani na wa kikosi cha uokoaji majeruhi hawajafika kwenye eneo la tukio. Theeastafrica imeendelea kuwasiliana na jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni ili kupata taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga amesema ajali hiyo ni mbaya na inafanana na ile ya Ubungo River Side!

Akisimulia zaidi kuhusiana na tukio hilo Kamanda Mpinga amesema lori la ng'ombe liliacha njia na kugongana na lori la mchanga ambalo lililivamia gari dogo lililoiparamia basi la abiria na kusababisha kifo vifo hivyo!

1 comment:

  1. BWANA ALITO NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIBARIKIWE. WAFIWA POLENI NA MUNGU AWATIE NGUVU KIPINDI CHOTE CHA MAJONZI.WALIOFARIKI WALIOKUWA WAMEJIANDAA KWA SAFARI YA MBINGUNI MLALE MAHALI PEMA PEPONI.AMINA

    KWA TULIOBAKI MUNGU ATUPE NEEMA YA KUJIANDAA KWA KUFUATA TARATIBU NA SHERIA ZA MUNGU. TUSICHOKE KUOMBA NA KUUTAFUTA USO WAKE KILA WAKATI.

    ReplyDelete