Wednesday, December 21, 2011

UMOJA WA WAHUTUBU WA DINI YA KIISLAM WASEMA MAANDAMANO KUPINGA USHARIKA WA SERIKALI NA MAKANISA YAKO PALE PALE!

Siku moja baada ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ALHAD MUSSA SALUM kutangaza kuzuia maandamano yaliyopangwa kufanywa na Waislamu kote nchini Umoja wa Wahutubu wa dhehebu hilo umeibuka na kupinga vikali karipio hilo huku ukisema maandamano hayo yatafanyika kama yalivyopangwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa umoja huo Sheikh KONDO BUNGO amesema maandamano hayo si kwa ajili ya kupinga Mahakama ya kadhi pekee kama ilivyonukuliwa na Sheikh Mkuu na badala yake yana malalamiko wanayotaka wayafikishe kwa serikali.

No comments:

Post a Comment