Chama Cha Kijamii CCK kimeungana na wadau wengine wa siasa nchini kukitaka Chama cha NCCR – Mageuzi kuangalia upya maamuzi ya kumfukuza Uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini DAVID KAFULILA pamoja na wanachama wengine watatu.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama hicho, Bwana CONSTANTINE AKITANDA, amesema endapo chama hicho hakitatafakari upya juu ya maamuzi hayo kitahakikisha kinampigania Mbunge huyo kwa namna yoyote ile ili kumwezesha kurudi Bungeni.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo ameitaka Serikali kutoafiki ongezeko la posho za wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba endapo italifumbia macho jambo hilo itakuwa haijawatendea haki Watanzania.
No comments:
Post a Comment