Utafiti uliofanywa na mkakati wa UWEZO TANZANIA, kunzia mei mwaka huu, kwa watoto zaidi ya laki moja na ishirini na nane elfu umebainisha kuwa watoto walio wengi nchini bado hawana uwezo wa kujumlisha, kusoma na kuandika.
Akiizungumzia ripoti hiyo, Jijini Dar es salaam, Mratibu wa utafiti wa UWEZO, Dkt. GRACE SOKO, amesema utafiti huo ulihusisha uwezo wa kusoma somo la kiingereza, Kiswahili pamoja na hisabati kwa watoto wenye umri kuanzia miaka saba hadi kumi na sita.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Bumbuli, JANUARY MAKAMBA, amesema uhaba wa Walimu nchini bado ni changamoto kubwa inayoikabili Serikali kufuatia Ripoti ya mkakati wa UWEZO TANZANIA kubainisha kuwa wastani wa watoto 63 katika shule za msingi nchini wanahudumiwa na mwalimu mmoja.
No comments:
Post a Comment