Thursday, March 8, 2012

WANAWAKE WATAKIWA KUWAPA HAKI SAWA WATOTO WA KIKE!

IMEBAINIKA kwamba Wanawake ndiyo vinara wa unyanyasaji wa watoto nchini licha ya kwamba wao ndiyo wenye jukumu zito la kubeba mimba na kuwazaa. Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo kitaifa ilifanyika jijini Arusha, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Sophia Simba alisema Wanawake ndiyo wanyanyasaji wakubwa wa watoto nchini.


“Leo hii tunasherehekea siku ya Wanawake Duniani lakini sisi ndiyo wanyanyasaji wa kubwa wa watoto, ingawa sisi ndiyo wenye jukumu la kubeba mimba miezi tisa na kuzaa, na baada ya kuwaleta Watoto hao Duniani tunaanza tena kuwanyanyasa”alisema Waziri Simba nakuongeza: “Kupitia siku hii muhimu Wanawake tunapaswa kujirekebisha katika suala hilo na badala yeke tuwalee watoto wetu katika mazingiza sahihi na yenye maadili mema huku tukiwaonyesha upendo”.
Alisema kama mwanamke atajitambua kuwa yeye ni mtu muhimu katika maisha yanayomzunguka hakutakuwa na suala la unyanyasaji wa watoto ambalo mwisho wake huchangia utitiri wa watoto wa mitaani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadiq alisema Wanawake ni watu wa muhimu sana nanikichocheo kikubwa cha maendelea ya ukuaji wa familia pamoja na uchumi wan chi kwa ujumla.


Alisema wanawake wanapaswa kujitambua na kujikita katika suala zima la maendeleo ya familia zao pamoja na maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Katika maadhimisho hayo ambayo hufanyika March 8 kila mwaka yalibeba ujumbe mzito wa mchakato wa katiba mpya.


Vyama mbalimbali vya wanawake pamoja na Wizara na Idara za Serikali zilizofanya maandamano kuanzia maeneo ya Kidonge Chekundu hadi katika Viwanja vya Mnazi mmoja vilikuwa na mabango mbalimbali yaliyozungumzia mchakato wa katiba.
Mabango hayo yalielezea umuhimu wa mwanamke kupewa kipaumbele katika masuala mbalimbali ya uongozi,utawala,uzalishaji mali katika kuleta maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment