Tuesday, November 22, 2011

VODACOM MISS TANZANIA SALHA ISRAEL AKABIDHI FULANA 1000 KWA MKOA WA RUKWA NA KATAVI!

Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akifurahia jambo wakati akimkabidhi fulana Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom imekabidhi fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne kusaidia hamasa ya tamasha hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole(kulia) akiangalia na kuifurahia moja kati ya fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne aliyokabidhiwa na Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel kushoto kwa ajili ya kufanikisha tamasha la utamaduni wa mkoa wa Rukwa na mkoa tarajiwa wa katavi litakalofanyika ijumaa katika kijiji cha makumbusho jijini Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim.
Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole kulia akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa katavi litakalofanyika ijumaa katika kijiji cha makumbusho mara baada ya Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel(katikati) kumkabidhi msaada wa fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne zilizotolewa na Vodacom Tanzania,kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim.
Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akifurahia jambo wakati akimkabidhi fulana Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi John Kafuku, Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom imekabidhi fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne kusaidia hamasa ya tamasha hilo.
Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akimkabidhi fulana Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole. Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim,wengine kutoka kulia Katibu wa kamati hiyo Godffrey Arubano na makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo John Kafuku Vodacom imekabidhi fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne kusaidia hamasa ya tamasha hilo.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu kushoto na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Salum Mwalim wakijadili jambo na Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel wakati wa makabidhiano ya fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne zilizotolewa na Vodacom Tanzania,kwa ajili ya kufanikisha tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi litakalofanyika ijumaa katika kijiji cha makumbusho jijini Dares salaam.

No comments:

Post a Comment