Tuesday, November 22, 2011

HALMASHAURI YA ILALA YAKABILIWA NA UHABA WA MADARASA 747, NYUMBA ZA WALIMU 3244!

Licha ya kampuni ya Simu za mkononi ya TIGO kutoa msaada wa madarasa mawili kwa shule ya msingi Pugu kajiungeni iliyoathiriwa na milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi iliyopo Gongo la mboto jijini Dar es Salaam, bado kuna uhaba wa madarasa 747,upungufu wa nyumba za waalimu 3244 pamoja na madawati 18,000 kwa shule zilizopo ndani ya halmshauri ya manispaa ya Ilala.

Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Manispaa ya Ilala ABILAH MCHIA amesema Kutokana na changamoto mbalimbali kumesababisha walimu kushindwa kufundisha vizuri na hatimaye kiwango cha Ufaulu kushuka.


Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Mkoa kutoka Tigo, ALEX MSIGARA amesema kampuni ya Tigo ipo mstari wa mbele katika kuchangia elimu ambapo maendeleo yanayopatikana duniani husababishwa na elimu.

No comments:

Post a Comment