Hii ni nyumba ya kiongozi wa dini wa kanisa la Kilokole inayodaiwa kutumika kwa imani za kishirikina na wakazi wa mji wa Iringa eneo la Frelimo ikiwa imevunjwa mara baada ya wananchi kuivamia.
Gari ya kiongozi wa dini wa kanisa la Kilokole inayedaiwa kuwa na imani za kishirikina na wakazi wa mji wa Iringa eneo la Frelimo ikiwa imevunjwa baada ya wananchi hao kuingia na kutaka kuichoma moto.
Huu ndio umati wa wakazi wa eneo la Flerimo waliofika kwenye nyumba ya kiongozi wa kidini wa kanisa la Kilokole wakimtuhumu kwa imani za kishirikina wakitawanyika baada ya kutawanywa na Polisi.
Huyu ndiye askari aliyejeruhuwa baada ya tukio hilo akipelekwa Hospitali kupatiwa matibabu.
NA FRANCIS GODWIN, Iringa.
Zaidi ya watu 10 wakiwemo askari wanne na wanahabari wamejeruhiwa huku baadhi yao wakitibiwa na kuruhusiwa na wengine kulazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kuibuka kwa mapigano hayo kati ya polisi na wananchi ,mapigano ambayo yametokana na imani potofu za wananchi katika kuamini ushirikina. Wananchi hao zaidi ya 200 walivamia nyumba ya mzee wa kanisa moja la kilokole katika mji wa Iringa eneo la Frelimo jina limehifadhiwa kwa sababu za kimaadili .
Hata hivyo pona ya wanahabari na polisi waliokuwa wamefungiwa ndani ya nyumba hiyo na kushambuliwa kwa mawe na kunusurika kuteketezwa kwa moto wakiwa ndani ya nyumba hiyo ilionekana baada ya askari polisi wa FFU kutumia mbinu kubwa ya kulazimika kutumia risasi ya moto kumshambulia mguuni mmoja kati ya watu wanaodaiwa kutaka kuongoza wengine kuichoma moto nyumba hiyo iliyokuwa na wahahabari ndani ,polisi na mchungaji mmoja .
Baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa kuokoa maisha ya wanahabari hao na watu wengine zaidi ya 10 ambao walipaswa kuuwawa na wananchi hao .
Wananchi hao walionekana kuongezeka idadi baada ya FFU kuwatisha kwa mabomu ya machozi huku wakidai kuwa mabomu hayo hayaui na bila polisi kupata mbinu ya haraka ya kutumia risasi ya moto zaidi ya watu hao 10 wakiwemo wanahabari waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wangekuwa wameuwawa na wananchi hao ambao waliondoa imani na kikosi hicho kuwa wamehusika kuificha misukule hiyo.Habari na Picha Hisani ya blog ya Francis Godwin!
No comments:
Post a Comment