Tuesday, November 22, 2011

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM CHAENDELEA MJINI DODOMA!

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea mjini Dodoma ambapo ajenda ya kukifanya chama kiondokane na utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini imechukua nafasi kubwa zikiwemo ajenda nyingine za kutekeleza maazimio ya kikao kilichopita.
Kikao hicho kilichogubikwa na usiri mkubwa kilianza leo asubuhi na kudumu kwa zaidi ya saa sita kabla ya kuahirishwa kwa mapumziko ya muda mfupi na hivi sasa kinaendelea na hakijulikani kitaisha muda gani kutokana na ajenda zilizopo kuwa ni nyingi kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho NAPE NNAUYE.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuahirishwa kwa muda kwa kikao hicho NAPE amesema uvumi unaoenezwa kuhusu ajenda za kikao hicho ikiwemo suala la kujivua Gamba kwa baadhi ya wanachama wake siyo sahihi na kuwa jambo hilo halijazungumziwa katika kikao chao ambacho kinajadili mambo mengine ya kukihusu chama na maandalizi ya ajenda za Halmashauri Kuu (NEC), itakayokutana kwa siku mbili kuanzia kesho.


Aidha Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema katika kikao hicho pia wamefanya uteuzi wa makatibu wapya kumi wa wilaya na kutengua uteuzi wa makatibu watatu wa wilaya ambao watapangiwa kazi nyingine.

No comments:

Post a Comment