Jukwaa la Katiba Tanzania limeahirisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Novemba 26, mwaka huu yaliyolenga kumsihi Rais JAKAYA KIKWETE asitie saini Muswada wa Sheria ya mabadiliko ya Katiba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jukwaa la Katiba kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Bw. DEUS KUBAMBA hatua hiyo inafuatia Jeshi la Polisi kuwaomba kusitisha maandamano hayo kwa vile Jeshi hilo limepokea maombi mengi ya makundi mbalimbali ya kijamii na kiasa kutaka kufanya maandamano nchi nzima siku hiyo na hivyo kuleta mkanganyiko.
Hata hivyo taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo na nia ya maandamano ya Jukwaa hilo yako pale pale na kuwa litapanga tarehe rasmi itakayotangazwa tena kwa wananchi baada ya mawasiliano na Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment