Thursday, November 24, 2011

SERIKALI YA UINGEREZA YATOA PAUNDI MILIONI 4 KUISAIDIA TANZANIA SENSA YA MAJARIBIO!

Serikali ya Uingereza imeongeza msaada wake wa paundi milioni nne na nusu kwa Serikali ya Tanzania ili kusaidia maandalizi ya zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26, mwaka 2012.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha, MUSTAFA MKULO, amesema fedha hizo zitasaidia zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi zaidi na serikali ya Tanzania imetenga jumla ya shilingi bilioni 50 katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2011/2012 kwa ajili ya maandalizi ya zoezi hilo.


Kwa upande wake Balozi wa Uingereza, nchini, DIANE CORNER, amesema zoezi la Sensa ya watu na makazi lina mchango mkubwa kwa Serikali kutathimini utekelezaji wa majukumu yake.

No comments:

Post a Comment