BENDI inayoendelea kufanya vizuri katika jukwaa la muziki wa dansi nchini Mapacha Watatu na Bendi Kongwe nchini, Msondo Ngoma zimeandaa shoo maalum kwa ajili ya kuwasindikiza ndugu zao kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taab (T-Moto) ‘Real Madrid’ katika uzinduzi wa kundi hilo utakaofanyika Oktoba 28 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akizungumza na Sufianimafoto, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa tayari maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na mazungumzo na bendi hizo zitakazowasindikiza katika onyesho hilo la uzinduzi ambazo zote zimeitikia wito.
Aidha Amini, alisema kuwa uzinduzi wa kundi hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa albam yao kwanza ya inayokwenda kwa jina la Aliyeniumba Hajanikosea. Kundi hilo tayari limekwisha kamilisha albam mbili kwa mpigo, ambapo itakayozinduliwa siku hiyo ya oktoba 28, tayari nyimbo zake zimeshaanza kupigwa katika vituo mbalimbali vya redio.
No comments:
Post a Comment