Sunday, July 31, 2011

WARAKA WA JOHN MNYIKA KWA WADAU NA WANAHARAKATI!

Natoa mwito wa Kituo Cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC), Jukwaa la Katiba, wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuelekeza nguvu katika hatua ya sasa kutaka muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ulioandikwa upya kuwekwa hadharani hivi sasa.

Muswada mbovu wa sheria ya mabadiliko ya katiba utatuletea katiba bomu isiyo na uhalali wa kukubaliwa na umma na kuongeza mpasuko katika nchi badala ya kuwa na muafaka wa kitaifa na misingi muhimu ya uwajibikaji kwa ustawi wa wote.

No comments:

Post a Comment