MADIWANI wa Chama cha Demekrasia na Maendeleo CHADEMA,leo wamesusia kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Singida, na kutoka nje, wakidai kukiukwa kwa kanuni za kudumu za uendeshaji wa vikao.
Wakiongozwa na mbunge wa Singida mashariki TUNDU LISSU ,wameeleza kusikitishwa na tabia ya kupitisha maamuzi muhimu, bila ya kupata muda wa kutosha, kwa ajili ya majadiliano.
Bwana LISSU amesema ,dosari hiyo isipotafutiwa ufumbuzi, wataendela kutoka nje siku ya kikao, ili dunia ielewe jinsi taratibu na sheria za baraza hilo zinavyokiukwa.
No comments:
Post a Comment