Sunday, October 16, 2011

VODACOM YASHIRIKI MKUTANO WA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA!


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia moderm ya intaenti ya kampuni ya Vodacom wakati Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Salum Mwalim akimpatia maelezo ya moderm hizo,wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Vodacom katika maonesho ya bidhaa na huduma pembezoni mwa mkutano wa wadau wa uwekezaji eneo la ziwa Tanganyika unaofanyika Mjini Mpanda. Mkutano huo utafunguliwa kesho 17 Oktoba, 2011 na Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Salum Mwalim akimsikiliza kwa umakini kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa SACP Isunto Mantage wakati wawili hao walipokutana katika banda la Vodacom katika maonesho ya wadau watakaoshiriki mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika mjini Mpanda. Mkutano huo unafanyika kesho 17 Oktoba, 2011 Mjini Mpanda, na utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete. Kampuni ya Vodacom imefadhili chakula cha mchana na cha usiku kwa wajumbe zaidi ya mia nne watakaohudhuria mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dk. Rajab Rutengwe akivutiwa na bidhaa mbalimbali za kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom katika banda la kampuni hiyo kwenye maoenesho ya wadau wa uwekezaji yanayofanyika mjini Mpanda. Mkutano huo unalenga kuongeza uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanyanyika unafanyika kesho 17 Oktoba, 2011 na utafunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.Vodacom imegharamia chakula cha mchana na usiku kwa washiriki wa mkutano huo.

Na Theeastafrica Bloger



Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom inashiriki mkutano wa uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika ulioanza leo mjini Mpanda kwa maonesho ya bidhaa na huduma kutoka wadau mbalimbali wa uwekezaji nchini.


Akitoa maelezo ya huduma na bidhaa za Vodacom kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyetembelea banda la Vodacom katika maonesho hayo Meneja Mawasiliano wa Vodacom Bw. Salum Mwalim amemueleza Bw. Pinda kuwa Vodacom inaunga mkono juhudi za serikali katika kuinua kiwango cha uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tangayika. Bw. Mwalim amemweleza Waziri Mkuu Pinda kuwa inaunga mkono juhudi za serikali za kushawishi uwekezaji katika eneo hilo hatua ambayo itasaidia kuinua uchumi wa mikoa ya Tabora, Kigoma na Rukwa pamoja na ustawi wa jamii za wakazi wa mikoa hiyo.


“Vodacom siku zote tunafurahia maendeleo ya nchi na wananchi na tumekuwa washirika wa maendeleo kwa vitendo, tumekuwa tukifanya juhudi za makusudi katika kubadili maisha ya watanzania kupitia tekenolojia ya simu za mkononi kupitia shabaha yetu ya kuwaunganisha watu, kutengeneza fursa na kubadili maisha”Alisema Bw. Mwalim. Meneja huyo wa Mawasiliano wa Vodacom ameongeza kuwa Vodacom tayari imeshawekeza kwa kiasi kikubwa katika ukanda huo hivyo kutoa uhakika wa mawasiliano wa sauti na data kwa wawekezaji wote watakaojitokeza kama ambavyo wananchi na wadau wengine wanavyofurahia mawasiliano ya mtandao huo wa Vodacom hivi sasa.


“Mh. Waziri Mkuu kama tunavyotambua biashara katika ulimwengu wa sasa unahitaji sana huduma ya uhakika wa mawasiliano hivyo hatua yetu ya kuwekeza katika ukanda huu bila shaka yatasaidia juhudi za serikali za kuhamasisha uwekezaji katika eneo hili”Aliongeza Mwalim na kuungwa mkono na Waziri Mkuu Pinda. “Ni kweli huduma za mawasiliano ni muhimu sana Vodacom mnafanya vizri wananchi wanapata huduma za simu ukanda huu wa ziwa Tanganyika ila ongezeni juhudi”Alisema Waziri Mkuu Pinda akiwa katika banda la Vodacom


Kampuni ya Vodacom ndio yenye mtandao mkubwa zaidi wa mawasiliano ya simu za mkononi katika ukanda wa ziwa Tanganyika kwa huduma zake kuwafikia wakazi wengi zaidi. Katika kuunga mkono juhudi za serikali zenye kulenga kuongeza kiwango cha uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika mbali na kushiriki mkutano huo Vodacom imedhamini chakula cha mchana na cha usiku kwa wajumbe zaidi ya mia nne wanaohudhuria mkutano huo.



No comments:

Post a Comment