Kukosekana kwa mikopo ya nyumba nchini kumetajwa kusababisha kuwepo kwa mifumo isiyo rasmi ya ujenzi na ununuzi wa nyumba hususani baada ya kufa kwa Benki ya nyumba Tanzania THB mwaka 1995.
Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji saini makubaliano kati ya Benki na Shirika la Nyumba la Taifa NHC ili kuwezesha kutoa mikopo ya nyumba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof ANNA TIBAIJUKA amesema kutokuwepo kwa mikopo ya nyumba kimeachangia kuathiri uchumi wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Bw NEHEMIAH MCHECHU amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kutachangia upatikanaji wa maendeleo kwenye sekta tatu.
No comments:
Post a Comment