Shirika lisilokuwa la kiserikali la Under The Same Sun limetoa msaada wa miwani kwa watu 204 wenye uono hafifu hususani watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na wengine 45 kupewa vifaa maalum vya kukuzia maandishi mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa shirika hilo nchini Tanzania Vick Mtetema amesema kuwa shirika lake limefarijika sana kukamilisha ahadi hiyo lililoiweka mwezi wa sita mwaka huu kama sehemu ya kuwawezesha katika elimu wanafunzi wenye uono hafifu ambao wamekuwa wakitengwa na wamekuwa wakitaabika kuona katika kujisomea au wakati wa mafunzo darasani.
No comments:
Post a Comment