Wednesday, September 7, 2011

TMA YATABIRI UWEPO WA MVUA ZA KUTOSHA KWENYE MAENEO MENGI NCHINI!

Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) imedai kwamba kunatarajiwa kuwa na mvua za kutosha katika maeneo mengi nchini hivyo wakulima ,wafugaji wameshauriwa kuanza kujitayarisha ili kuweza kukabiliana na madhara yeyote yatakayoweza kutokea kutokana na mvua hizo.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo DKT AGNES L.KIJAZI amesema hasa katika maeneo ambayo yatakuwa na mvua nyingi wakulima na wafugaji wanapaswa kufuata ushauri wa maafisa ugani katika maeneo yao ili kupata mbinu mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo pamoja na kuzitumia mvua hizo kwa ajili ya kuboresha mifugo na mazao shambani.


Dokta KIJAZI ameongeza kuwa mvua hizo za vuli zitakazoanza OCTOBA mpaka DESEMBA mwaka huu zitasababisha ongezeko la maji katika mabwawa mengi nchini.

No comments:

Post a Comment