Sunday, September 25, 2011

DK ALLI MOHAMED SHEIN AZINDUA SHULE YA WASICHANA YATIMA NA WANAOTOKA KWENYE MAZINGIRA MAGUMU 'WAMA NAKAYAMA'!

Rais wa Zanzibar DK ALLI MOHAMED SHEIN akielekezwa jambo na mmoja ya wanafunzi wa shule ya Sekondari WAMA NAKAYAMA.
Rais wa Zanzibar DK ALLI MOHAMED SHEIN akielekezwa jambo na mmoja ya wanafunzi wa shule ya Sekondari WAMA NAKAYAMA.

Baadhi ya wageni waalikwawakisikiliza maelezo ya jinsi ya kutumia Computer na Projector kutoka kwa  mmoja ya wanafunzi wa shule ya Sekondari WAMA NAKAYAMA.

Rais wa Zanzibar DK ALLI MOHAMED SHEIN akiwa chumba cha maabara hapa, shule hii ni ya mchepuo wa Sayansi......sikiliza muheshimiwa hapa ndipo tunapofanyia uchunguzi wa hiki na kile ndivyo anavyoonekana kusema mmoja ya wanafunzi wa shule ya Sekondari WAMA NAKAYAMA.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar DK MOHAMED SHEIN amesema kufunguliwa kwa shule ya Sekondari ya wasichana yatima na wale wanaosihi kwenye mazingira magumu ya WAMA NAKAYAMA iliyopo Nyamisati Kibiti Rufiji Mkoani Pwani kutatoa fursa kwa watoto hao kutimiza ndoto zao za kimaendeleo.


Na Mwandishi Wetu


Akifungua rasmi shule hiyo ya sekondari WAMA NAKAYAMA, DK MOHAMED SHEIN amesema watoto wengi wa kike hususani wanaoishi kwenye mazingira magumu hukatishwa masomo kutokana na dhana ya kihistoria kwamba wasichana ni mitaji ya wazazi katika kujipatia fedha za mahari.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA, Mama SALMA KIKWETE amesema kufunguliwa kwa shule hiyo kumempa faraja katika harakati zake za kuwakomboa watoto wa kike walioshindwa kuendelea na masomo kupata fursa hiyo.

No comments:

Post a Comment