Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limewaomba wawekezaji wa sekta ya umeme nchini Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Limited (PAT) ambayo inajihusisha na usambazaji wa gesi asilia kujitokeza kwa wananchi na kueleza bayana kuhusika na tatizo la mgao wa umeme.
Akizungumza na kituo hiki Meneja uhusiano wa TANESCO, BADRA MASOUD amesema kutokana na Kampuni hiyo kutoisambazia TANESCO gesi ya kutosha hali hiyo imesababisha makali ya mgao wa umeme nchini huku malalamiko ya Wananchi yakielekezwa kwenye Shirika hilo.
No comments:
Post a Comment