Sunday, September 25, 2011

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE CAMBRIDGE WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU!


Wahitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Cambridge wakiingia rasmi katika sherehe za mahafali yao kwa wimbo maalum. Sherehe hizo zilifanyika Shuleni hapo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali pamoja na ndugu na jamaa.
Pichani Juu na Chini Mgeni rasmi Hoyce Temu akiwapa risala wahitimu wa kidato cha IV katika shule ya Cambridge. Hoyce aliwasihi wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanafanya mitihani yao kwa utulivu na kujiamini sambamba na kuwasisitiza kuchagua masomo yenye masoko katika ajira na kujiendeleza binafsi. Aidha aliwaomba wazazi na walezi kuwasaidia vijana hao katika safari yao ya Maisha na kuwataka kuwa wavumilivu wakati wote ili waweze kufikia mafanikio.
Naye mwanafunzi Rose Nawander akipokea cheti cha kuwa mwanafunzi bora kwa upande wa taaluma na vilabu vya dini kutoka kwa mgeni rasmi Hoyce Temu.
Umati wa wageni waalikwa, walezi na wazazi waliohudhuria mahafali hayo ya kumi na moja shuleni hapo.
JAPO NI KIDOGO TUNAKUOMBA UZIWASILISHE KWA SESILIA, ndivyo anavyosema Meneja wa Shule ya Sekondari Cambridge Bi. Laura Mataita wakati akimakabidhi mgeni rasmi na Mwendeshaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Bi. Hoyce Temu.

No comments:

Post a Comment