Sunday, September 25, 2011

WAATHIRIKA WA MABOMU GONGOLAMBOTO WALALAMIKIA KUTOONA MAJINA KWENYE ORODHA YA WATAKAOLIPWA!

Baadhi ya Waathirika wa Mlipuko wa Mabomu uliotokea februali 16, mwaka huu katika kambi ya Jeshi la wananchi, Gongo la Mboto, Jijini Dar es salaam wameilalamikia Serikali kufuatia kutoona majina yao ya ulipwaji wa fidia kwenye orodha iliyotolewa katika Ofisi ya kata hiyo.

Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamehoji kitendo cha serikali kutoa malipo kwa waathirika wa vyombo vya ndani huku ikiwaacha wale waliobomolewa makazi yao ambao kwa sasa hawajui hatima ya muda wa kuishi kwenye mahema.


Kwa upande wake Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala ELLIOTHI MWASABWITE amekiri kupokea malalamiko hayo na kuwataka wakazi hao wawe na subira na kudai kuwa majina hayo bado yanaendelea kutolewa.

No comments:

Post a Comment