Mbunge wa Same Mashariki ANNE KILANGO MALECELA amepinga majibu yaliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kuhusiana na utekelezwaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na kusema ni ya udanganyifu.
Akizungumza Bungeni mjini Dodoma Mheshimiwa ANNE KILANGO amebainisha kuwa miradi iliyotajwa kutekelezwa na serikali ilikamilika kutokana na ufadhili na hivyo amehoji lini atapewa ahadi zinazotekelezeka ikiwemo kuwachukulia hatua watendaji waliotoa taarifa hizo.
Akijibu tuhuma hizo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, AGGREY MWANRI amesema ametoa jibu hilo baada ya utekelezaji wa miradi ya hiyo kuthibitishwa na Mkurugenzi mtendaji na Mhandisi wa maji.
No comments:
Post a Comment