Tuesday, May 10, 2011

HOSPITALI YA AMANA KUHUDUMIA WAGONJWA KUMI WA UPASUAJI KWA SIKU!

                                     MUSSA HASSAN ZUNGU, Mbunge wa Ilala
                                                         Bango la Hospitali ya Amana
Majengo ya Hospitali ya Amana
Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam sasa itakuwa na uwezo wa kufanyia upasuaji wagonjwa zaidi ya kumi kwa siku mara baada ya kuzinduliwa kwa wodi inayotoa huduma hiyo iliyojengwa kwa msaada wa Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Umoja wa Nchi za Ulaya EU na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Akizungumza wakati wa Uufunguzi wa Wodi hiyo Mbunge wa Jimbo la Ilala MUSSA HASSAN ZUNGU amezitaka Manispaa za Kinondoni na Temeke kuiga mfano huo ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupatiwa huduma mbalimbali za upasuaji.
                                                MESHACK SHIMWELA (Katikati)
Kwa Upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dakta MESHACK SHIMWELA amesema ujenzi huo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 28 utaongeza idadi ya wagonjwa watakaopatiwa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment