Thursday, August 18, 2011

VIZIMBA MACHINGA COMPLEX VYAWA GUMZO, WAFANYABIASHARA WASEMA WANAVIMILIKI KIHALALI!


Ikiwa ni siku moja baada ya Meya wa Jiji la DSM, Dakta DIDAS MASABURI kutoa maamuzi ya kuwasimamisha baadhi ya wamiliki wa vizimba walioingia kinyume na utaratibu katika soko la Machinga Complex, wameibuka na kudai kwamba wapo kisheria na kutaka suala hilo lisitumiwe kwa minajili ya Ki-siasa.

Wakizungumza na kituo hiki Wamiliki hao wamedai kwamba vizimba hivyo wamekuwa wakivimiliki kihalali huku wakiitaka Serikali kuingilia kati mzozo huo ili kuepusha hali ya uvunjifu wa amani unaoweza kutokea wakati wowote.


Nae Mwenyekiti wa soko la Machinga Complex ABUBAKAR RAKESH amesema wanasiasa wamekuwa wakilitumia kwa lengo la kujikweza ki-siasa hali ambayo inaweza kuharibu utaratibu mzuri na mipangilio ya soko hilo.

No comments:

Post a Comment